Ushahidi mpya unaonyesha kwamba jeshi la Rwanda
linawasaidia waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hii ni kwa
mujibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights
Watch.Shirika hilo limesema waasi wa zamani wameelezea jinsi Rwanda
iliwasajili wapiganaji kujiunga na waasi pamoja na kutoa silaha.
Rwanda pia imedaiwa kutoa hifadhi kwa Jenerali
muasi Bosco Ntaganda,anayetakikana na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu
wa kivita ICC. Serikali ya Rwanda imekanusa kuwafadhili waasi hao.Waandishi wa habari wamesema japo ripoti hii haijailaumu moja kwa moja serikali ya Rwanda kwa kuwafadhili waasi, hata hivyo imeutaka utawala wa Kigali kuhakikisha vitendo vya kuwasajili wapiganaji na kuvukisha silaha vinadhibitiwa.
Maasi yanayoendelea Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanaongozwa na Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye zamani alikuwa kamanda katika kundi la waasi wa CNDP lakini baadaye lilijumuishwa katika jeshi la Congo mwaka 2009 kufuatia mkataba wa amani.
Na BBC
No comments:
Post a Comment