Aliyeshinda
ni Ndg. Amos Majile Kanuda (Mwenyekiti wa CCM Wilaya) na Ndg. Yasin
Said Membar (MNEC) yani Mjumbe wa NEC, na pia Ndg. Richard Mayunga (amechaguliwa kuwa
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya, Siasa, Itikadi na Uenezi, na
Ndg. Majaliwa Bilal Ismail amechaguliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu
ya CCM Wilaya ya Nzega, Uchumi na Fedha
Kwa hali hiyo matokeo yalikuwa hivi...!!
Kanuda
alipata kura 1486, Francisko Kulwa Shija kura 588, Patrick Joseph
Bulabuza kura 38 , kwa nafasi ya Uenyekiti na MNEC sikumbuki kura zao
ila waligombea watu watatu Emmanuel Misigalo, Yassin Said Membar na Paul
Kabelele, uchaguzi wa kwanza aliongoza Misigalo akafuatiwa na Membar
lakini hakuvuka nusu hivyo ngoma ikarudiwa, na hapo ndipo Membar
aliposhinda kwa kura zaidi ya 1000 na mwenzake Misigalo alipobaki na
ushindi wa kura 400 na ushee
Na hivi ndivo alivyoandika katika ukurasa wake wa FB Mbunge wa Nzega baada ya matokeo hayo...!!!
Mara
baada ya fununu za matokeo ya uchaguzi kuwa wazi kuna watu wawili
maarufu walizimia, na walipozinduka waliangua vilio na hawajaonekana
Nzega tena...tunawapa pole na kuwatakia quick recovery huko waliko! Huo
ndiyo ushindani...na sisi tunawaambia kuwa wasihofu kitu watatendewa
haki siku zote katika chama hiki na katika uongozi huu. Malengo yetu
ilikuwa ni kuondoa watu wa hovyo, wachumia tumbo n
a
wanaofanya kazi kwa maelekezo ya mtu mmoja tu na sasa kuweka watu
makini na mahiri watakaokisimamisha chama, hata kama itamaanisha
kuniadhibu mimi pale itakapobidi...Chama Kwanza, Mtu baadaye! Hakuna mtu
maarufu na wa maana ndani ya CCM kuliko CCM yenyewe. Nimesikia wanataka
kuikimbia nchi, tunawasihi wasifanye hivyo, waendelee tu kuwa waadilifu
na waaminifu kwa chama na kwa nchi na ipo siku mambo yao yatawanyookea
tu!
Muheshimiwa mbunge amekuwa akisimama kidete tangu uchaguzi umeanza mpaka matokeo hayo kutoka ninguvu yake ya na ukomavu wake wa Siasa umetoa majibu haya.
Mh, Hamisi Kigwangalla
No comments:
Post a Comment