Mwendesha mashtaka mkuu wa
mahakama ya jinai ya kimataifa- ICC, Fatou Bensouda leo amesema kwamba
mahakama hiyo iko tayari kushauriana na Kenya kisheria kuhusu ombi la
kutaka kesi inayowakabili rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta na naibu
wake, William Ruto kuhamishiwa nyumbani.
Tamko hilo linatolewa wiki moja tu baada ya
viongozi wa Umoja wa Afrika kutoa wito kwa ICC irejeshe kesi za Uhuru na
Ruto zishughulikiwe nchini Kenya.Alisema kwa mujibu wa mkataba wa Roma ambao ndio msingi wa mahakama ya ICC, nchi yoyote inayotaka kesi irejeshwe yafaa itosheleze kwa majaji wa ICC kwamba itaendeleza mashtaka hayo hayo kwa watuhumiwa.
Bi Bensouda alisema ICC ni mahakama huru ambayo haiegemei misingi ya kisiasa na majaji wake hutoa uamuzi bila kushurutishwa na yeyote.Alisema ICC itaendelea kushirikiana na mataifa 34 yaliyosaini mkataba wa kujiunga na mahakama hiyo.
Wiki jana, viongozi na serikali wanachama wa Umoja wa Afrika waliafikiana mjini Addis Ababa Ethiopia kwenye kongamano lao kwamba yafaa kesi zinazowakabili rais Uhuru Kenyatta, naibu wake, William Ruto pamoja na mwanahabari Joshua arap Sang zirejeshwe na kushughulikiwa nchini Kenya.
Uhuru na Ruto wameshtakiwa kwa kupanga na kufadhili mapigano ya baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2007, yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu na kuwaacha wengine takriban nusu milioni bila makao.
Na
BBC
No comments:
Post a Comment