Kituo cha televisheni cha Serikali ya Syria kinasema kuwa majeshi ya serikali yamethibiti mji wa Qusayr baada ya makabiliano makali kati yao na waasi nchini humo.
Ripoti kutoka kwa wapiganaji wanaopinga serikal zinasema kuwa wameamua kuondoka katika mji huo.
Kwa sasa mji huo ambao unadaiwa kumiliki barabara muhimu, umekuwa mahame kufuatia vita vikali vilivyochukuwa takriban majuma matatu kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa upinzani.
Tayari maelfu ya wapiganaji wa kundi la hezbollah kutoka lebanon wameungana na vikosi vya serikali ili kuthibiti mji huo.
Hatua hii inajiri wakati ambapo wajumbe kutoka umoja wa mataifa ,marekani na Urusi wanakutana mjini Geneva, Switzerland ili kujaribu kuzileta mezani pande zinazozozana.
Waasi wanasema kuwa walikuwa wameondoka
kutoka vijijini eneo la Kaskazini. Televisheni ya serikali ilisema kuwa
wanajeshi wa serikali na wale wa kundi la
Hezbollah, waliweza kuvamia mji.
Picha zilizopeperushwa kwenye televisheni zinaonyeshwa zilionyesha mji wa
Qusair ukiwa hauna watu. Taarifa zinasema
hatua ya kuuteka mji huo ni hatua nzuri kwa serikali kuuteka mji huo
ulio karibu na mpaka wa Lebanon.
No comments:
Post a Comment