Pages

Thursday, June 20, 2013

Mizengo Pinda: Chadema wanatekeleza kauli yao ya nchi haita tawalika.

Mhe Mizengo Pinda leo bungeni kwenye kipindi cha maswali na majibu ameeleza waziwazi kuwa kuna haja ya kuwakabili viongozi wa kisiasa.

Katika kulidadavua hilo ametolea mfano kauli ya Dr Slaa aliyoitoa baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu, kauli hiyo ni ile iliyosema "nchi haita tawalika".

Lakini pia ameongezea ya kuwa,"kama wananchi watakaidi kauli ya vyombo vya dola ya kuwataka waache vurugu, basi naagiza vyombo vya dola viwapige tu, kwani hatuwezi kuendelea hivi."

 Akijibu swali la mh mangungu,mb. Waziri mkuu mizengo pinda amesema matukio ya kigaidi na uvunjifu wa amani yanayoendelea hapa nchini hivi sasa ni mwendelezo na utekelezaji wa kauli ya nchi haitatawalika iliyotolewa na chadema baada ya kushindwa uchaguzi mkuu 2010 na wakati wanaingia bungeni walitoa kauli hiyo..pinda amesema serikali imevumilia vya kutosha sasa basi..dola iachwe ichukue hatua za kurudisha amani ya nchi kwani vita ikitokea hakuna atakayebaki salama, tutaathirika wote. Amesema atakayevunja sheria na kusababishwa vurugu lazima akutane na virungu vya polisi.

 Lakini pia ameongezea ya kuwa,"kama wananchi watakaidi kauli ya vyombo vya dola ya kuwataka waache vurugu, basi naagiza vyombo vya dola viwapige tu, kwani hatuwezi kuendelea hivi."

 My take. Sasa serikali ipo kazini kulinda na kudumisha amani. Tuipe ushirikiano

No comments:

Post a Comment