Pages

Saturday, September 7, 2013

DK, Hamisi Kingwangalla kavunja ukimya kuhusu Baba yake mzazi......!!!

DK, Hamisi Kigwangalla ni mbunge wa Jimbo la Nzega lakini pia ni Mwenyekiti wa TAMISEMI, Ameamua kusema yamoyoni na yaliyokuwa ndani ya familia yake hii nikutokana na Baadhi ya wanasiasa kuanza kumchafua kwa kusema anamtelekeza Baba yake mzazi, na wengine kusema HK sio mtanzania halisi bali nimkongo.
 HK kavunja ukimya jana baada kashfa hizo kuzidi kusambaa mitandaoni.
Lakini ikumbukwe kuwa kuwa HK akishafunguka ktk show moja ya Radio inaitwa MAKUTANO SHOW na Dada Fina Mango na sauti ya mahojiano hayo ipo mitandaoni.
Alianza kwa kusema hivi.

"Wanabodi, amani ya mungu na iwe juu yenu. Sijaisikia hiyo clip lakini hii mijadala imenifungua kidogo kuhusu nini mnaongea kuhusu mambo binafsi yangu na familia yangu. Kuna watu huamini kuwa ukiwa public figure unakuwa mali ya umma na hivyo ya kwako ya binafsi pia ni ya umma. Naamini nawajibika kutoa maelezo angalau kwa ufupi tu.


Fact one: story hii haina ukweli wa kutosha.

Fact two: story hii ina mkono wa watu wasionitakia mema na wenye nia ovu ya kunichafulia njia yangu ya maisha haya ya umma niliyoyachagua.

Fact 3: huyo ni baba yangu.

Fact 4: huyo si mama yangu. Mama yangu anaitwa Bagaile Bakari Lumola. Anaishi Tabora na ni mtumishi wa CCM wilaya ya Uyui.

Fact 5: Baba alinitelekeza kijijini kwao Goweko kwa babu yangu nikaugua Marasmic Kwashiakor nikanusurika kufa huku yeye akila maisha mjini (refer majibu yangu kwenye Show ya Makutano na Fina Mango, yapo mtandaoni), hakunilea, sikulelewa na baba wa kambo. Nililelewa na bibi na babu mzaa mama.

Fact 6: Baba yangu hakuchangia hata thumni kwenye elimu yangu wala hata maisha yangu.

Fact 7: Nimesoma na nasimamia misingi ya maadili ya dini yangu. Sina roho mbaya na ninasaidia watu baki wengi.

Fact 8: SIJAMTELEKEZA baba yangu. SIMLiPIZII KISASI wala siwezi kufanya hivyo. Hayo yalipita na mimi natimiza wajibu wangu leo kadri ninavyojaaliwa. Amefika hapo kwa kuwa ndipo alipopanga mwenyewe akiwa kijana. Watoto wake siyo mimi tu, anao na wengine kwa mama wengine. Amewafikisha wapi? Mbona hao hawasemi? Anawajibika kwa maisha yake mwenyewe. Anatibiwa na Madaktari bingwa mahiri na wabobezi kwenye hospitali 2, Heameda Medical Clinic (ipo scout - ni ya Dr. Mwandolela Heri (Rukoma unamfahamu, mpigie akupe file na bill utazame huwa zinalipwa na nani) - huyu ni daktari bingwa wa moyo na hii ni private clinic yake. Pia anatibiwa MNH, Cardiology Clinic Private na Dr. Tulizo Shemu (daktari bingwa wa moyo pia). Naamini pia Dr. Rukoma anamfahamu anawezasaidia jukwaa kwa kuweka kumbukumbu sahihi. Mpaka ninavyoongea hapa anaendelea na dawa za kila siku huku akisubiria rufaa ya kwenda kufanyiwa procedure nje. Kila mwezi anapata pesa zaidi ya 300,000 toka kwangu kwa ajili ya chakula na mengineyo, dawa zenye thamani ya zaidi ya 250,000. Na yeye mwenyewe si kiwete, ana elimu na uzoefu na naamini anafanya kazi zake na kujipatia chochote. Nimemfanyia vipimo vyenye thamani ya zaidi ya 2ml ikiwa ni pamoja na kumsaidia apate tiba first class na katika fast track.

Fact 9: Yeye walau ana hicho kibanda chake na huyo mkewe. Mimi binafsi sina hata nyumba moja iliyokamilika kabisa. Bado najenga. Japokuwa siku za usoni amekuwa akidai nimnunulie gari na nimjengee nyumba kubwa zaidi eti kwa kuwa mimi ni Mbunge sasa na ni tajiri. Ni kweli mimi ni Mbunge na nina hisa kwenye makampuni kadhaa lakini sina hela za kufanya yote haya kwa wakati mmoja huku nisomeshe wadogo zangu 6, watoto wangu wawili, wananzega karibu 600 na nifanye mengine ya kuendesha maisha yangu ya kila siku. Makampuni hayo nipo na wenzangu na hivyo siwezi kujichukulia tu fedha kutatua kero zangu binafsi. Ni mpaka nipewe gawio. Sasa hivi namjengea nyumba mama yangu na pia nimemnunulia gari ya kutembelea ili astaafu vizuri. Yeye nimempa kipaumbele kwa kuwa naye alinipa kipaumbele na kunionesha upendo na njia sahihi ya maisha. Siwezi kumlipa kwa chochote lakini nimedhamiria kwenda extra mile kumfurahisha maana ali-shade tears several times nikimuulizia kuhusu baba yangu yuko wapi wakati nikikua.

Fact 10: Mungu ndiye atatoa hukumu kama niko sawa ama nayumba ktk hili.

Fact 11: Nalazimika kuamini kuwa pengine afya ya akili ya baba yangu ina mashaka makubwa kwa sasa. Ana sahau ya ajabu. Hana insight tena maskini. Siku vijana hawa walipokwenda kuzungumza naye, aliwaomba 20,000 wakati mimi jana yake tu nilikuwa nimemtumia 50,000 kwa njia ya m-pesa. Ni juzi tu (miezi miwili na ushee iliyopita) nimekutana naye Dodoma na Mhe. Mng'ong'o akamtambulisha kwa heshima kubwa mbele ya wabunge wenzangu tuliokuwa tukihudhuria semina ya UKIMWI pamoja pale St. Gaspar. Na kila nilipopata mtoto nilimpelekea. Mara ya mwisho HK Jr kazaliwa Februari 2013. Na kila siku ya clinic dereva wangu humfuata mpaka kule Pugu Kinyamwezi na kumleta hospitali. Ni mimi mwenyewe niliyempeleka kwa hao madaktari. Ni mke wangu aliyesimamia vipimo na consultation zote za hospitali. Mke wangu huenda na watoto mpaka kule na mafurushi ya vyakula na kushinda the whole day.

Nimalizie kwa kusema; msituone wanadamu tunatembea na kucheka. Ni kwa vile kuna historia za maumivu zilizojificha katika maisha yetu ndani ya subconscious mind, vinginevyo tungeya-process yote haya tungechanganyikiwa. Kuna watu hawalali wakinitafuta. Sintowalipizia kisasi japokuwa nayajua ya kwao ya aibu. Kwenye siasa kuna limits za kufanya mambo hata kama mtu huyo hakupendi. Sikumsema vibaya kiasi hicho Mhe. Mbowe na naamini hakuchukia kiasi cha kuhangaika na mimi. Hawa ni wanaCCM wenzangu wenye nia ovu.

Nimeyasema yote haya ili iwe wazi toja kwangu na watu wasipate taabu ku-speculate maana naamini ipo siku umma wa waTanzania utanipa mahukumu makubwa zaidi ya haya na hivyo sina sababu ya kuficha chochote".


Wakatabahu,
HK.

www.peterdafi.blogspot.com nitazidi kuwaletea habari hizi kiundani na soon ntazileta Clip za Sauti na video za muunganiko wa Story hii.
pia unaweza mpata HK katika mitandao yote kwa Jina la HAMISI KIGWANGALLA.

No comments:

Post a Comment