Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto ambaye pia ni Mwenyekiti
wa UWT-TAIFA Sophia Simba amewataahadhalisha vijana na wananchi wa Mbozi
ktk mji wa Tunduma kujiepusha na vurugu na uvunjaji wa amani unaofanywa
na chama cha Chadema.
Amewaambia wananchi wajiepushe na Chadema kwani kimefanya mauawaji ya
wananchi ktk miji ya Iringa,Morogoro,Arusha na Igunga- Tabora,akaenda
mbali kwa kuwaambia wananchi kuwa CCM inajua CHADEMA inatumiwa na
mataifa ya nje kuanzisha vita Tanzania ili mataifa hayo yapate mahali na
soko la kuuza silaha,anasema hayo ndo yalitokea Misri,Libya,Tunisia na
sasa Syria.
Mama Simba akawambia vijana wajiulize ni kwanini ktk hayo mauwaji
hayajafanyika Moshi,na kwanini hakuna maandamano ktk mkoa
K'njaro?kawatahadhalisha vijana wa Tunduma kuachana na CHADEMA kwani
wataishia kufa na kuandamana pasipo sababu.
Mama Sophia Simba yupo ktk ziara wilaya ya Mbozi na wilaya mpya ya Mwomba kuimalisha Chama chake.
No comments:
Post a Comment