Ziara ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK
WILBROAD SLAA katika mikoa ya Singida, Shinyanga, Kigoma na Tabora
ambayo ilitarajiwa kuanza tarehe 3 Desemba 2013 na kumalizika tarehe 23
Desemba 2013 inatarajiwa kugharibu shilingi Milioni 19,833,300/=.
Gharama hizo ni pamoja na posho ya Dr Slaa (80,000 x siku 22 =
TSH.1,760,000), posho kwa wana timu 7 (40,000 x siku 22 x watu 7 =
TSH.6,160,000), mafuta kwa ajili ya magari 3 (lita 2071 x 2300 = TSH.
4,763,300), vikao vya ndani 19 (TSH. 1,900,000), posho ya waandishi wa
habari na watangazaji wa ITV, Nipashe, Mwananchi, Star TV na Tanzania
Daima (TSH. 4,550,000), matengenezo ya Gari la ALLAN (TSH. 730,000),
Batery za Megaphone ya Katibu Mkuu (TSH 300,000) pamoja na Dharura na
Uratibu (TSH. 450,000).
Katika ziara hiyo, Dk Slaa atazungumzia mambo yafuatayo;
- Mambo yaliyoibuliwa na CAG ambayo taarifa zake zitajadiliwa bungeni
- Ripoti ya CHC kuhusu ubinafsishaji wa makampuni
- Ripoti maalum ya uchunguzi wa Spika kuhusu posho za wabunge
- Posho ya Kamati Maalum za Bunge
- Harufu ya ufisadi kwenye mradi wa maji Singida
Chanzo:- Jamii Forum (Chabruma)
No comments:
Post a Comment