Pages

Sunday, December 29, 2013

Mauwaji ya Kutisha Iringa


Yametokea mauwaji ya kutisha ktk Kijiji cha Migoli ktk wilaya ya Iringa vijijini,mauwaji hayo yametokana na wivu wa Kimapenzi.
Akiongea na Radio Ebony Fm ya mkoani Iringa,Mwenyekiti wa kijiji cha Migoli ndugu Alamu Mbilinyi amesema mauwaji hayo yametokea siku ya Ijumaa 27/12/2013,ambapo mwanaume anayejulikana kwa jina la Alex Mwanawandembo(34) mkazi wa kijiji hicho amemchinja mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Anna (23) na kutenganisha kolomeo na kiwiliwili na kisha kumfunika marehemu na blanketi kitandani kwa sababu tu ya wivu mapenzi.
Wakielezea tukio hilo mashuhuda na wakazi wa kijiji cha Migolo,wamesema ndugu Alex alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke huyo kwa mda,baada ya mwanamke huyo kuachika kwa mume wake,mahusiano yao yalikuwa na ugomvi wa hapa na pale baada ya mara kadhaa ndugu Alex kumtuhumu mpenzi wake kukosa uaminifu,hali hiyo ilimuumiza mwanaume aliyeonekana kumpenda kwa dhati.
Siku ya tukio,ndugu Alex ambaye na yeye kwa sasa ni marehemu,alimchinja mpenzi wake wakiwa chumbani,ambapo alimpitishia kisu shingoni na kukata koromeo na tena kumkata sehemu ya mdomoni hadi usawa wa taya,kisha kumfunika na kuingia mtaani.
Aliondoka hadi kwa mama yake na kumwachia kiasi cha pesa ya sikukuu,akamtembelea bibi yake na kumpa kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya kupata kinywaji cha komoni na baadae kuaga kuwa anaenda mtoni kuoga,baadae alipita kwa marafiki zake akiwalalamikia kuwa kuna mtu amemuudhi na atamfanyia kitu kibaya,wakati hayo yakiendelea maiti ya mwanamke ilikuwa chumbani bila majirani kujua.
Baadae Marehemu Alex alirudi nyumbani kwake alipopanga,akawaaga majirani kuwa anahama na kwenda mjini Iringa,anaenda kufunga ndoa ya milele na mpenzi wake Anna...na hawezi kurudi tena na kufanya kazi ya uvuvi ktk bwawa la Mtela,baadae akaenda dukani akanunua dawa ya panya,viroba aina ya vodka na konyagi akanywa huku akijifungia na maiti.
Majirani walishtushwa na sauti ya kukoroma,wakavunja mlango na kujaribu kumnywesha maziwa lkn haikusaidia,na ktk kufunufunua wakagundua na mwili wa mwanamke uliochinjwa kama kuku,marehemu wote wamezikwa ktk makabuli ya kijiji cha Migoli.
Akiongea Mwenyekiti wa Kijiji cha Migoli bwana Alamu Mbilinyi amesema tukio hilo ni la aina yake na halijawahi kutokea kijijini hapo,wamezoea kupatwa na majanga ya watu kuliwa na mamba au viboko ndani ya maji,watu kujinyonga au kuuliwa na tembo porini na si kuchinjana.Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa upelelezi unaendelea.

No comments:

Post a Comment