Pages

Wednesday, December 11, 2013

Siri ya Tata Madiba na Tanzania Yetu

"Tusisubiri CNN Waiambie Dunia Mchango Wa Tanzania Kwa Ukombozi Wa Afrika...!

Kazi hiyo tuifanye sisi wenyewe. Jana usiku sana nilimwona Rais wa Ghana John Dramani Mahama akihojiwa na CNN kuhusiana na Mandela. Mara tatu Rais huyo wa Ghana aliutaja mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Afrika ikiwemo Afrika Kusini ya Nelson Mandela.

-Hivi ni wangapi wanajua kuwa kiongozi wa kwanza wa chama cha ukombozi katika nchi huru ya Kiafrika ambaye Mandela alikutana nae anaitwa John Mwakangale. Huyu alikuwa kiongozi katika TANU na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

-Hivi ni wangapi wanajua kuwa Mji wa kwanza katika nchi huru ya Kiafrika ambayo Mandela alikanyaga ardhi yake unaitwa Mbeya. Hivyo basi, Tanganyika ndio nchi huru ya kwanza ya Kiafrika ambapo Mandela alikanyaga ardhi yake.

- Hivi ni wangapi duniani wanajua, kuwa Julius Nyerere ndiye Rais wa kwanza katika nchi huru ya Kiafrika ambaye Mandela alikutana nae. Na ni Julius Nyerere baada ya kumkubali Mandela, ndiye aliyemsaidia Mandela kwa kumtambulisha kwa Mfalme Haille Selassie wa Ethiopia?

Haikuwa ajabu, kuwa baada ya kutoka gerezani, kwa Mandela Tanzania ikawa nchi ya kwanza kuitembelea.

Kumbukumbu hizi muhimu za kihistoria na nyinginezo Watanzania hatupaswi kuisubiri CNN na vyombo vingine vya habari vya kimagharibi viitangazie dunia.

Ni jukumu letu wenyewe".

No comments:

Post a Comment