Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili
uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru
leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis
Mwamunyange.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga
21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo
uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya
Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52
ya Uhuru.Sehemu
ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa
ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo
leo jijini Dar es salaam.Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma
Kikwete akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za
maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo. Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.Rais
Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi
Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na
Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa
haraka.Baadhi
ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa
wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Wananchi
wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka
52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.Vijana
wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya
maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es
salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini,
Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”Vijana
wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana
mfano wa mnyama aina ya simba kuashiria utalii katika hifadhi za
wanyama za Tanzania.
Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa
maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya
kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Mzee
Nelson Rolihlahla Mandela Madiba aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya
Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa watanzania na
kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo
madarakani.Rais
wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi
Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa
na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa
Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.Raia
wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara
wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari
(MAELEZO) leo.Rais
Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis
Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na
Idara ya Habari (MAELEZO) leo.Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa
viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya
Uhuru.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
No comments:
Post a Comment