Pages

Thursday, February 13, 2014

Lowasa kumkabili kikwete dodoma

LOWASA KUMKABILI KIKWETE DODOMA
WAKATI wanasiasa waandamizi wanaotajwa kusaka urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiitwa kuhojiwa mjini Dodoma kuhusiana na ukiukwaji wa maadili, mmoja miongoni mwao anatajwa kutishia kukigawa na kumkabili mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, ambaye anadai amemsaliti katika alichokiita ahadi ya kumuachia nafasi yake 2015.
Taarifa za ndani ya kambi ya mwanasiasa huyo mwenye nguvu ndani ya CCM zinaeleza kwamba, maandalizi yameshaanza kufanyika kukabiliana na Mwenyekiti Rais Kikwete ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, kwa maelezo kwamba ndiko anakoamini kuwa na nguvu kubwa kuliko vikao vingine.
Pamoja na mmoja wa wasaidizi wake rasmi kukanusha taarifa hizo, anayetajwa ni Edward Lowassa, waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu baada ya kuhusishwa na sakata la mradi wa umeme wa dharura wa kampuni ya Richmond LLC.
Hoja kuu inayojengwa na kundi hilo ni kwamba, Rais Kikwete alisaidiwa kwa kiasi kikubwa kuingia madarakani na mgombea wao kwa ahadi kwamba angemuachia nafasi atakapomaliza muda wake mwakani 2015, jambo ambalo kwa sasa wanaona kama amewasaliti kwa kuanza kumdhibiti asiendelee na harakati zake za kusaka urais kupitia CCM.
Mbali ya matukio mengine kadhaa ya kisiasa, chanzo cha sintofahamu hiyo kimeelezwa kuwa ni kauli ya hivi karibuni ya Rais Kikwete kutaka kushughulikiwa kwa wanaotumia fedha kujitafutia madaraka na kukemea wanaojitangaza kuwania urais kabla ya chama kutoa kibali.
Tayari CCM imekwishaanza mchakato wa hatua hizo kwa kuwaita mbele ya Kamati Ndogo ya Maadili ya chama hicho, wanasiasa sita wanaotajwa kuwania urais kupitia chama hicho, akiwamo Lowassa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Wamo pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, wote wakihusishwa moja kwa moja na kuanza harakati za kusaka urais kupitia chama hicho kabla ya wakati.
Ndani ya kundi hilo ni wawili Lowassa na Membe ambao walikuwa pamoja na Kikwete katika mchakato wa kuwania urais kupitia CCM mwaka 2005, wakiwa katika kundi lililojipatia umaarufu kama ‘mtandao’, kundi ambalo kwa sasa limeshasambaratika na baadhi yao wakitajwa kuratibu uundwaji wa makundi mapya ya kimkakati.
Inaelezwa kwamba mmoja wa vinara hao amekwishaunda sekretarieti ambayo imeanza kazi ya kufanya kazi sambamba na ile rasmi ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, wakidai kwamba utaratibu huo ulitumika pia mwaka 2005 kumpitisha Kikwete.
“Mzee (anamtaja) ameunda sekretarieti na sasa inajipanga kuishika NEC na kwa kweli tutamsema Mwenyekuti kwamba hata yeye aliunda mtandao ambao ulimsaidia kuingia madarakani na sasa anasahau na kuunga mkono watu ambao hawajamsaidia lolote,” anaeleza mtoa habari wetu ndani ya kambi hiyo.
Msaidizi rasmi wa Lowassa, ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, alipoulizwa kuhusu madai hayo ya kambi ya Lowassa kuhusu Rais Kikwete kuwasaliti wanamtandao waliomsaidia kumwingiza madarakani, alisema madai yote hayo yanatengenezwa na wabaya wa Lowassa katika mkakati wao wa kutaka kumchonganisha na Rais Kikwete.
“Sikiliza ndugu yangu, hao wanaozusha hayo ni walewale ambao siku zote wamekuwa wakifanya juhudi kubwa za kumchonganisha (Lowassa) na Bwana Mkubwa (Rais Kikwete),” alisema na kuongeza:
“Walianza mwaka 2010 wakadai Lowassa atachukua fomu ya kugombea urais, mwaka 2012 wakaja na madai mengine kwamba Lowassa ameandaa mkakati wa kumvua kofia ya uenyekiti Kikwete ili abakie na urais, eti (Kikwete) ameonyesha ombwe la uongozi ndani ya Chama...
“Ninachojua mimi, wawili hawa bado wako pamoja, Rais Kikwete hajawahi kumsaliti wala kumtenga Lowassa kwa namna yoyote ile. Rais Kikwete bado ana imani naye sana (Lowassa), na hata juzi juzi ulisikia jinsi Rais Kikwete alivyosema ndani ya kikao cha NEC kwamba anamwamini Lowassa kwa hiyo wanamwachia kata ya Makuyuni, CCM isipeleke nguvu nyingine yoyote, Lowassa anatosha. Juzi tena hapa Rais Kikwete ametoa Sh bilioni 3.0 kwa ajili kuchimba mabwawa matatu ya maji Monduli ili kutatua kero ya maji katika eneo fulani ambako kulikuwa na kero ya maji…waambieni, mbinu zao hizo hazitafanikiwa.”
Hata hivyo, taarifa zinasema kwamba hali si shwari ndani ya kambi ya Lowassa na wafuasi wake wamekuwa wakitoa maneno makali dhidi ya Rais Kikwete na wasaidizi wake ndani ya CCM, akiwamo Makamu Mwenyekiti, Philip Mangula, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwa madai kwamba hawampendi mgombea wao.
Akizungumzia taarifa hizo, Nape aliliambia Raia Mwema kwamba CCM haigopi vitisho kutoka kwa mtu yeyote kwa maelezo kwamba chama hicho kinaendeshwa na vikao, Katiba, na kanuni na hivyo kila jambo linatekelezwa kwa haki na kisheria.
“Hakuna wa kutishia chama, chama ni taasisi na kinaendeshwa kwa vikao, katiba, sheria na kanuni na hivyo hakuna mwanachama aliye juu ya chama. Haiwezekani mwanachama akakiuka maadili halafu akatoa vitisho kupindisha maamuzi.
“Si busara sana kutishana. Kama mtu anataka nafasi si vyema kutishana. Ni sawa na mtu anataka kufanya mtihani wa CPA (Certified Public Accountant) lakini anawatisha wasimamizi ili wampitishe bila kufuata taratibu,” anasema Nape.
Kiongozi mwingine wa CCM mkoani Dar es Salaam ameliambia Raia Mwema kwamba mwaka 1995 kuliwahi kutokea tishio la kuihusisha NEC kumtetea mmoja wa wagombea urais aliyekataliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye alikemea na kutoa mfano wa mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
Kuitwa kwa wana CCM wanaoonyesha kuwania urais 2015 kupitia chama hicho, kunahitimisha matamko kadhaa ya chama hicho yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wake ndani na nje ya vikao, lakini kumekuwa na uzito katika kuchukua hatua.
Kamati hiyo ndogo ya maadili itakayowahoji wanaotaka urais inaundwa na Mangula, Kinana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Shamsi Vuai Nahodha, Dk. Maua Daftari na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana.
Vikao vya CCM vimeanza jana kwa Kamati Kuu (CC) ya CCM, kukutana Dar es Salaam, NEC ya chama hicho ikitarajiwa kukutana Jumamosi na Jumapili wiki hii mjini Dodoma.
Vikao hivyo pamoja na mambo mengine vinatarajiwa kujadili ushiriki wa wajumbe wake katika Bunge Maalumu la Katiba ambalo limepangwa kuanza Februari 18, mwaka huu mjini Dodoma

Tomato source: Mwandishi wetu Raia Mwema 12-02-2014

- See more at: Raia Mwema - Lowassa kumkabili Kikwete Dodoma

No comments:

Post a Comment