Home »
siasa
» Lowasa kumkabili kikwete dodoma
Lowasa kumkabili kikwete dodoma
LOWASA KUMKABILI KIKWETE DODOMA
WAKATI
wanasiasa waandamizi wanaotajwa kusaka urais ndani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) wakiitwa kuhojiwa mjini Dodoma kuhusiana na ukiukwaji wa
maadili, mmoja miongoni mwao anatajwa kutishia kukigawa na kumkabili
mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, ambaye anadai amemsaliti
katika alichokiita ahadi ya kumuachia nafasi yake 2015.
Taarifa za ndani ya kambi ya
mwanasiasa huyo mwenye nguvu ndani ya CCM zinaeleza kwamba, maandalizi
yameshaanza kufanyika kukabiliana na Mwenyekiti Rais Kikwete ndani ya
kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, kwa maelezo
kwamba ndiko anakoamini kuwa na nguvu kubwa kuliko vikao vingine.
Pamoja na mmoja wa wasaidizi wake
rasmi kukanusha taarifa hizo, anayetajwa ni Edward Lowassa, waziri mkuu
wa zamani aliyejiuzulu baada ya kuhusishwa na sakata la mradi wa umeme
wa dharura wa kampuni ya Richmond LLC.
Hoja kuu inayojengwa na kundi
hilo ni kwamba, Rais Kikwete alisaidiwa kwa kiasi kikubwa kuingia
madarakani na mgombea wao kwa ahadi kwamba angemuachia nafasi
atakapomaliza muda wake mwakani 2015, jambo ambalo kwa sasa wanaona kama
amewasaliti kwa kuanza kumdhibiti asiendelee na harakati zake za kusaka
urais kupitia CCM.
Mbali ya matukio mengine kadhaa
ya kisiasa, chanzo cha sintofahamu hiyo kimeelezwa kuwa ni kauli ya hivi
karibuni ya Rais Kikwete kutaka kushughulikiwa kwa wanaotumia fedha
kujitafutia madaraka na kukemea wanaojitangaza kuwania urais kabla ya
chama kutoa kibali.
Tayari CCM imekwishaanza mchakato
wa hatua hizo kwa kuwaita mbele ya Kamati Ndogo ya Maadili ya chama
hicho, wanasiasa sita wanaotajwa kuwania urais kupitia chama hicho,
akiwamo Lowassa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),
Steven Wassira na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Wamo pia Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliyewahi kuwa Waziri wa
Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, January Makamba, wote wakihusishwa moja kwa moja
na kuanza harakati za kusaka urais kupitia chama hicho kabla ya wakati.
Ndani ya kundi hilo ni wawili
Lowassa na Membe ambao walikuwa pamoja na Kikwete katika mchakato wa
kuwania urais kupitia CCM mwaka 2005, wakiwa katika kundi lililojipatia
umaarufu kama ‘mtandao’, kundi ambalo kwa sasa limeshasambaratika na
baadhi yao wakitajwa kuratibu uundwaji wa makundi mapya ya kimkakati.
Inaelezwa kwamba mmoja wa vinara
hao amekwishaunda sekretarieti ambayo imeanza kazi ya kufanya kazi
sambamba na ile rasmi ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman
Kinana, wakidai kwamba utaratibu huo ulitumika pia mwaka 2005 kumpitisha
Kikwete.
“Mzee (anamtaja) ameunda
sekretarieti na sasa inajipanga kuishika NEC na kwa kweli tutamsema
Mwenyekuti kwamba hata yeye aliunda mtandao ambao ulimsaidia kuingia
madarakani na sasa anasahau na kuunga mkono watu ambao hawajamsaidia
lolote,” anaeleza mtoa habari wetu ndani ya kambi hiyo.
Msaidizi rasmi wa Lowassa, ambaye
hakupenda jina lake litajwe gazetini, alipoulizwa kuhusu madai hayo ya
kambi ya Lowassa kuhusu Rais Kikwete kuwasaliti wanamtandao
waliomsaidia kumwingiza madarakani, alisema madai yote hayo
yanatengenezwa na wabaya wa Lowassa katika mkakati wao wa kutaka
kumchonganisha na Rais Kikwete.
“Sikiliza ndugu yangu, hao
wanaozusha hayo ni walewale ambao siku zote wamekuwa wakifanya juhudi
kubwa za kumchonganisha (Lowassa) na Bwana Mkubwa (Rais Kikwete),”
alisema na kuongeza:
“Walianza mwaka 2010 wakadai
Lowassa atachukua fomu ya kugombea urais, mwaka 2012 wakaja na madai
mengine kwamba Lowassa ameandaa mkakati wa kumvua kofia ya uenyekiti
Kikwete ili abakie na urais, eti (Kikwete) ameonyesha ombwe la uongozi
ndani ya Chama...
“Ninachojua mimi, wawili hawa
bado wako pamoja, Rais Kikwete hajawahi kumsaliti wala kumtenga Lowassa
kwa namna yoyote ile. Rais Kikwete bado ana imani naye sana (Lowassa),
na hata juzi juzi ulisikia jinsi Rais Kikwete alivyosema ndani ya kikao
cha NEC kwamba anamwamini Lowassa kwa hiyo wanamwachia kata ya Makuyuni,
CCM isipeleke nguvu nyingine yoyote, Lowassa anatosha. Juzi tena hapa
Rais Kikwete ametoa Sh bilioni 3.0 kwa ajili kuchimba mabwawa matatu ya
maji Monduli ili kutatua kero ya maji katika eneo fulani ambako kulikuwa
na kero ya maji…waambieni, mbinu zao hizo hazitafanikiwa.”
Hata hivyo, taarifa zinasema
kwamba hali si shwari ndani ya kambi ya Lowassa na wafuasi wake wamekuwa
wakitoa maneno makali dhidi ya Rais Kikwete na wasaidizi wake ndani ya
CCM, akiwamo Makamu Mwenyekiti, Philip Mangula, Katibu Mkuu Abdulrahman
Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwa madai kwamba
hawampendi mgombea wao.
Akizungumzia taarifa hizo, Nape aliliambia Raia Mwema
kwamba CCM haigopi vitisho kutoka kwa mtu yeyote kwa maelezo kwamba
chama hicho kinaendeshwa na vikao, Katiba, na kanuni na hivyo kila jambo
linatekelezwa kwa haki na kisheria.
“Hakuna wa kutishia chama, chama
ni taasisi na kinaendeshwa kwa vikao, katiba, sheria na kanuni na hivyo
hakuna mwanachama aliye juu ya chama. Haiwezekani mwanachama akakiuka
maadili halafu akatoa vitisho kupindisha maamuzi.
“Si busara sana kutishana. Kama
mtu anataka nafasi si vyema kutishana. Ni sawa na mtu anataka kufanya
mtihani wa CPA (Certified Public Accountant) lakini anawatisha
wasimamizi ili wampitishe bila kufuata taratibu,” anasema Nape.
Kiongozi mwingine wa CCM mkoani Dar es Salaam ameliambia Raia Mwema
kwamba mwaka 1995 kuliwahi kutokea tishio la kuihusisha NEC kumtetea
mmoja wa wagombea urais aliyekataliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye alikemea na kutoa mfano wa mke
wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
Kuitwa kwa wana CCM wanaoonyesha
kuwania urais 2015 kupitia chama hicho, kunahitimisha matamko kadhaa ya
chama hicho yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wake ndani na nje ya
vikao, lakini kumekuwa na uzito katika kuchukua hatua.
Kamati hiyo ndogo ya maadili
itakayowahoji wanaotaka urais inaundwa na Mangula, Kinana, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi,
Shamsi Vuai Nahodha, Dk. Maua Daftari na Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana.
Vikao vya CCM vimeanza jana kwa
Kamati Kuu (CC) ya CCM, kukutana Dar es Salaam, NEC ya chama hicho
ikitarajiwa kukutana Jumamosi na Jumapili wiki hii mjini Dodoma.
Vikao hivyo pamoja na mambo
mengine vinatarajiwa kujadili ushiriki wa wajumbe wake katika Bunge
Maalumu la Katiba ambalo limepangwa kuanza Februari 18, mwaka huu mjini
Dodoma
Tomato source: Mwandishi wetu Raia Mwema 12-02-2014
WAKATI wanasiasa waandamizi wanaotajwa kusaka urais ndani ya Chama
cha Mapinduzi (CCM) wakiitwa kuhojiwa mjini Dodoma kuhusiana na
ukiukwaji wa maadili, mmoja miongoni mwao anatajwa kutishia kukigawa
na kumkabili mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, ambaye
anadai amemsaliti katika alichokiita ahadi ya kumuachia nafasi yake
2015.
Taarifa za ndani ya kambi ya mwanasiasa huyo mwenye nguvu ndani ya
CCM zinaeleza kwamba, maandalizi yameshaanza kufanyika kukabiliana na
Mwenyekiti Rais Kikwete ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC) ya chama hicho, kwa maelezo kwamba ndiko anakoamini kuwa na nguvu
kubwa kuliko vikao vingine.
Pamoja na mmoja wa wasaidizi wake rasmi kukanusha taarifa hizo,
anayetajwa ni Edward Lowassa, waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu baada
ya kuhusishwa na sakata la mradi wa umeme wa dharura wa kampuni ya
Richmond LLC.
Hoja kuu inayojengwa na kundi hilo ni kwamba, Rais Kikwete
alisaidiwa kwa kiasi kikubwa kuingia madarakani na mgombea wao kwa
ahadi kwamba angemuachia nafasi atakapomaliza muda wake mwakani 2015,
jambo ambalo kwa sasa wanaona kama amewasaliti kwa kuanza kumdhibiti
asiendelee na harakati zake za kusaka urais kupitia CCM.
Mbali ya matukio mengine kadhaa ya kisiasa, chanzo cha sintofahamu
hiyo kimeelezwa kuwa ni kauli ya hivi karibuni ya Rais Kikwete kutaka
kushughulikiwa kwa wanaotumia fedha kujitafutia madaraka na kukemea
wanaojitangaza kuwania urais kabla ya chama kutoa kibali.
Tayari CCM imekwishaanza mchakato wa hatua hizo kwa kuwaita mbele
ya Kamati Ndogo ya Maadili ya chama hicho, wanasiasa sita wanaotajwa
kuwania urais kupitia chama hicho, akiwamo Lowassa, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri Mkuu
Mstaafu, Frederick Sumaye.
Wamo pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe, aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William
Ngeleja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January
Makamba, wote wakihusishwa moja kwa moja na kuanza harakati za kusaka
urais kupitia chama hicho kabla ya wakati.
Ndani ya kundi hilo ni wawili Lowassa na Membe ambao walikuwa
pamoja na Kikwete katika mchakato wa kuwania urais kupitia CCM mwaka
2005, wakiwa katika kundi lililojipatia umaarufu kama ‘mtandao’, kundi
ambalo kwa sasa limeshasambaratika na baadhi yao wakitajwa kuratibu
uundwaji wa makundi mapya ya kimkakati.
Inaelezwa kwamba mmoja wa vinara hao amekwishaunda sekretarieti
ambayo imeanza kazi ya kufanya kazi sambamba na ile rasmi ya CCM
inayoongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, wakidai kwamba
utaratibu huo ulitumika pia mwaka 2005 kumpitisha Kikwete.
“Mzee (anamtaja) ameunda sekretarieti na sasa inajipanga kuishika
NEC na kwa kweli tutamsema Mwenyekuti kwamba hata yeye aliunda mtandao
ambao ulimsaidia kuingia madarakani na sasa anasahau na kuunga mkono
watu ambao hawajamsaidia lolote,” anaeleza mtoa habari wetu ndani ya
kambi hiyo.
Msaidizi rasmi wa Lowassa, ambaye hakupenda jina lake litajwe
gazetini, alipoulizwa kuhusu madai hayo ya kambi ya Lowassa kuhusu
Rais Kikwete kuwasaliti wanamtandao waliomsaidia kumwingiza madarakani,
alisema madai yote hayo yanatengenezwa na wabaya wa Lowassa katika
mkakati wao wa kutaka kumchonganisha na Rais Kikwete.
“Sikiliza ndugu yangu, hao wanaozusha hayo ni walewale ambao siku
zote wamekuwa wakifanya juhudi kubwa za kumchonganisha (Lowassa) na
Bwana Mkubwa (Rais Kikwete),” alisema na kuongeza:
“Walianza mwaka 2010 wakadai Lowassa atachukua fomu ya kugombea
urais, mwaka 2012 wakaja na madai mengine kwamba Lowassa ameandaa
mkakati wa kumvua kofia ya uenyekiti Kikwete ili abakie na urais, eti
(Kikwete) ameonyesha ombwe la uongozi ndani ya Chama...
“Ninachojua mimi, wawili hawa bado wako pamoja, Rais Kikwete hajawahi
kumsaliti wala kumtenga Lowassa kwa namna yoyote ile. Rais Kikwete
bado ana imani naye sana (Lowassa), na hata juzi juzi ulisikia jinsi
Rais Kikwete alivyosema ndani ya kikao cha NEC kwamba anamwamini
Lowassa kwa hiyo wanamwachia kata ya Makuyuni, CCM isipeleke nguvu
nyingine yoyote, Lowassa anatosha. Juzi tena hapa Rais Kikwete ametoa
Sh bilioni 3.0 kwa ajili kuchimba mabwawa matatu ya maji Monduli ili
kutatua kero ya maji katika eneo fulani ambako kulikuwa na kero ya
maji…waambieni, mbinu zao hizo hazitafanikiwa.”
Hata hivyo, taarifa zinasema kwamba hali si shwari ndani ya kambi ya
Lowassa na wafuasi wake wamekuwa wakitoa maneno makali dhidi ya Rais
Kikwete na wasaidizi wake ndani ya CCM, akiwamo Makamu Mwenyekiti,
Philip Mangula, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye kwa madai kwamba hawampendi mgombea wao.
Akizungumzia taarifa hizo, Nape aliliambia Raia Mwema kwamba
CCM haigopi vitisho kutoka kwa mtu yeyote kwa maelezo kwamba chama
hicho kinaendeshwa na vikao, Katiba, na kanuni na hivyo kila jambo
linatekelezwa kwa haki na kisheria.
“Hakuna wa kutishia chama, chama ni taasisi na kinaendeshwa kwa
vikao, katiba, sheria na kanuni na hivyo hakuna mwanachama aliye juu ya
chama. Haiwezekani mwanachama akakiuka maadili halafu akatoa vitisho
kupindisha maamuzi.
“Si busara sana kutishana. Kama mtu anataka nafasi si vyema
kutishana. Ni sawa na mtu anataka kufanya mtihani wa CPA (Certified
Public Accountant) lakini anawatisha wasimamizi ili wampitishe bila
kufuata taratibu,” anasema Nape.
Kiongozi mwingine wa CCM mkoani Dar es Salaam ameliambia Raia Mwema
kwamba mwaka 1995 kuliwahi kutokea tishio la kuihusisha NEC kumtetea
mmoja wa wagombea urais aliyekataliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye alikemea na kutoa mfano wa
mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
Kuitwa kwa wana CCM wanaoonyesha kuwania urais 2015 kupitia chama
hicho, kunahitimisha matamko kadhaa ya chama hicho yaliyokuwa
yakitolewa na viongozi wake ndani na nje ya vikao, lakini kumekuwa na
uzito katika kuchukua hatua.
Kamati hiyo ndogo ya maadili itakayowahoji wanaotaka urais inaundwa
na Mangula, Kinana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu
na Bunge), William Lukuvi, Shamsi Vuai Nahodha, Dk. Maua Daftari na
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana.
Vikao vya CCM vimeanza jana kwa Kamati Kuu (CC) ya CCM, kukutana Dar
es Salaam, NEC ya chama hicho ikitarajiwa kukutana Jumamosi na
Jumapili wiki hii mjini Dodoma.
Vikao hivyo pamoja na mambo mengine vinatarajiwa kujadili ushiriki wa
wajumbe wake katika Bunge Maalumu la Katiba ambalo limepangwa kuanza
Februari 18, mwaka huu mjini Dodoma
- See more at: Raia Mwema - Lowassa kumkabili Kikwete Dodoma
Post a Comment