Inspekta Jenerali wa Polisi
(IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa,
wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja
na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la
Polisi. Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni
pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi
mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi
mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna
msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa
Ruvuma. Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna
msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,
aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi
(ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa
Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi
(ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi. Zaidi ya hao
wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa
Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda
kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa upelelezi
Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga
anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa
Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Bwire,
anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora . Aidha, aliyekuwa afisa
Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Kauga
anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa
wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu
wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa kikosi
cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu
wa upelelezi mkoa wa Pwani. Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa
Usalama Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa
Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye
amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa
Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji anakwenda
kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP)
Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa
Trafiki mkoa wa Temeke. Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa
Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa
Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu
wa Polisi (SP) Meloe Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa
Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi
wa Polisi (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa
wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, Mrakibu Msaidizi
wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa
wa Ilala. Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu
na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi
wanaendelea kupata huduma bora ya usalama. Imetolewa na: Advera
Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi
No comments:
Post a Comment