Wakuu,
Wakati Serikali ikidaiwa kushindwa kuwalipa watumishi wake mshahara wa
mwezi Januari 2014 mpaka sasa, kuna tetesi kuwa Waziri wa Fedha
aliyeteuliwa na Mhe. Rais hivi karibuni Mhe. Saada Mkuya amewaandalia
wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti ya Bunge pamoja na maofisa waandamizi
kutoka Wizara ya Fedha safari ya kufanya 'utalii' kwenye nchi za Sweden
ama Norway kwa muda wa siku zaidi ya kumi kama njia ya
kujipongeza na kuwaweka sawa wabunge hao kwa bajeti atakayoiwasilisha
katikati ya mwaka huu. Safari hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya tarehe
02 - 12 Februari, 2014.
Safari hiyo iliyobatizwa 'Study Tour' kwa ajili ya kujenga uwezo
kwenye mambo ya bajeti na ukusanyaji wa mapato itajumuisha ujumbe wa
watu zaidi ya thelathini ambao watagharamiwa kila kitu na Wizara ya
Fedha ama Hazina jambo linaloonekana kuwa ni staili nyingine ya kutoa takrima kwa wabunge ili wapitishe bajeti za wizara
husika bila mikingamo mingi baada ya staili aliyotumia aliyekuwa Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kwa wakati huo Bw. Jairo kugundulika
hali iliyosabisha kupoteza nafasi yake.
Jambo la kujiuliza ni kuwa; inakuwaje Serikali inalalama kila siku kuwa
haina fedha jambo linalopelekea kushindwa kulipa hata mishahara ya
watumishi wake kwa wakati lakini inakuwa na uwezo wa kugharamia safari
zisizokuwa na tija kwa taifa na ambazo zinagharimu mamilioni ya fedha za
walipa kodi?
(Nusanusa
yetu imepata viambatanishi kadhaa kama uthibitisho wa kinachojiri ndani
ya Wizara ya Fedha katika suala hilo ikiwemo barua na orodha ya
wanaotakiwa kusafiri pasipo kujumuisha maofisa wengine ambao wako kwenye
level ya chini)
CHANZO:- Jamii Forum
No comments:
Post a Comment