Kundi la mataifa saba
yaliyostawi zaidi kiviwanda almaarufu kama G7 limelaani vikali hatua za
kijeshi zilizochukuliwa na Urusi nchini Ukraine-viongozi kundi hilo
wakitaja hatua ya Urusi kama ukiukaji wa uhuru wa Ukraine.
Katika taarifa ya pamoja iliyotiwa pia saini na
Umoja wa Ulaya EU-Urusi imetakiwa kushughulia wasiwasi wake kuihusu
Ukraini kupitia mashauri au upatanishi.Kundi hilo la mataifa saba tajiri zaidi duniani maarufu kama G-Seven limesema kuwa linachukuwa uamuzi wa kuahirisha matayarisho ya kongamano ambalo lingefanyika nchini Urusi mwezi juni mwaka huu kutokana na vitendo vya Moscow. Taarifa hiyo inakuja wakati vikosi vya Urusi vikiimarisha uthibiti katika rasi ya crimea ambapo Urusi inasema kuwa inalinda raia wake baada ya serikali kupinduliwa mjini Kiev.
Mbunge mashuhuri wa Urusi - Vyacheslav Nikonov, ameimabia BBC kwamba Urusi imejiandaa kwenda vitani kulinda maslahi yake nchini Ukraine na hususan katika mji wa Sevastopol.
"Ukraine ilialikwa kujiunga na Nato na hii ina maana kuwa marekani, au vituo vyake vya kijeshi vitawekwa nchini Ukraine. Urusi itafanya lolote, itahatarisha kuingia vita kuzuia hilo kutokea. Ni kuhusu kituo cha kijeshi, ni kuhusu mustakabal wa Urusi, mustakabal wa Ukraine. Sidhani kama mataifa ya magharibi yanaelewa kwamba Ukraine ni mahali ambapo Urusi ilizaliwa," amesema Nikonov.
"Tunatoa wito kwa urusi kuheshimu ahadi zake za kimataifa, kuondoa vikosi vyake na kujiepusha na uvamizi katika maeneo mengine nchini Ukraine. Tunatowa wito kwa pande zote kufuata njia ya amani katika kusuluhisha mgogoro huo kupitia mazungumzo, kupitia wachunguzi wa kimataifa chini ya mwavuli wa umoja wa baraza la usalama la umoja wa mataifa au shirika la ushirikiano wa kiusalama ulaya OSCE,'' amesema bwana Rasmussen.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani , John Kerry, anatarajiwa kuzuru Kiev hapo kesho jumanne kuiunga mkono serikali mpya ya Ukraine.
Haya yanajiri wakati mkuu wa jeshi la wanamaji wa Ukraine, Denis Berezovsky, akipokonywa madaraka yake baada ya kusema hadharani kwamba anaunga mkono serikali mpya ya Jimbo la Crimea ambayo inaunga mkono Urusi. Serikali ya Kiev imesema kuwa inamfanyia uchunguzi kwa nia ya kumfungulia mashtaka ya uhaini.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment