Pages

Wednesday, July 16, 2014

Mkataba wa muda wa Kusitisha Vita Gaza



Mkataba wa muda wa kusitisha vita Gaza


Vuguvugu la kupigania Uhuru wa Palestina, Hamas, na Israel zimekubali kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza kwa muda wa saa tano baadaye hivi leo baada ya siku tano za mapigano makali.
Baada ya ombi la umoja wa mataifa jeshi la Israel limesema kuwa litasitisha mashambulizi kati ya saa nne asubuhi hadi saa tisa kwa saa za Gaza, ili kuwaruhusu wakaazi kupata chakula na huduma muhimu.
Makubaliano ya kusitisha vita ni ya mda, Hamas inadai hoja zao hazijatiliwa maanani
Msemaji wa Hamas Sami Abu Zukhri amethibitisha kuwa vuguvugu hilo kadhalika litasitisha mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel wakati huo.
Msemaji wa shirika la umoja wa mataifa linalowasaidia wakimbizi wa Palestina Christopher Gunnes amesema kuwa ni matumaini yake kwamba usitishaji huo wa mapigano utatoa fursa ya kusuluhisha matatizo yanayoikabili gaza.
Hapo jana jumatano jazba zilizidi pale watoto wanne wa kipalestina wote kutoka familia moja waliuwawa katika shambulizi la mizinga kutoka Israel wakati wakicheza kwenye ufuo wa bahari huko Gaza.
Israel imesema ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa Hamas na kwamba vifo hivyo ni matokeo ya mkasa mkubwa wa mapigano hayo.
Naye rais wa Marekani Barrack Obama amesisitiza kuwa Israel ina haki ya kujilinda.

Maombolezi,Mama wa moja wa watoto waliouliwa katika shambulio la Israel huko Gaza

No comments:

Post a Comment