Mkataba wa muda wa kusitisha vita Gaza
Vuguvugu la kupigania Uhuru wa Palestina, Hamas, na
Israel zimekubali kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano katika
ukanda wa Gaza kwa muda wa saa tano baadaye hivi leo baada ya siku tano
za mapigano makali.
Baada ya ombi la umoja wa mataifa jeshi la
Israel limesema kuwa litasitisha mashambulizi kati ya saa nne asubuhi
hadi saa tisa kwa saa za Gaza, ili kuwaruhusu wakaazi kupata chakula na
huduma muhimu.Msemaji wa shirika la umoja wa mataifa linalowasaidia wakimbizi wa Palestina Christopher Gunnes amesema kuwa ni matumaini yake kwamba usitishaji huo wa mapigano utatoa fursa ya kusuluhisha matatizo yanayoikabili gaza.
Hapo jana jumatano jazba zilizidi pale watoto wanne wa kipalestina wote kutoka familia moja waliuwawa katika shambulizi la mizinga kutoka Israel wakati wakicheza kwenye ufuo wa bahari huko Gaza.
Israel imesema ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa Hamas na kwamba vifo hivyo ni matokeo ya mkasa mkubwa wa mapigano hayo.
Naye rais wa Marekani Barrack Obama amesisitiza kuwa Israel ina haki ya kujilinda.
Post a Comment