Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji akishuka baada ya kumuokoa mtoto
eneo la Mabatini, jijini Mwanza lililokumbwa na mafuriko baada ya Mto Mirongo
kufurika kutokana na mvua iliyonyesha jana. Hii Picha na Michael Jamson
Mwanza. Baadhi ya wakazi wa Kata ya Mbugani, Mtaa wa
Mbugani A na B wameathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na
mvua kubwa iliyonyesha jana kwa saa nne.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema mvua
hiyo imesababisha vitu vyao kusombwa na maji na nyumba
kubomoka.
Esther Misanga, mkazi wa mtaa huo, alitaja baadhi ya vitu
vilivyoharibiwa na mvua hiyo kuwa ni magunia 20 ya mahindi,
magunia 10 ya daga na mifuko 20 ya unga wa sembe, vyote
vikiwa na thamani ya jumla ya Sh2 milioni.
“Nimepoteza magunia 50 ya mahindi na unga wa dona.
Nimepata hasara kubwa sana. Sikutegemea yangetokea mafuriko
makubwa kama haya,” alisema Misanga.
Alisema Serikali iliwaahidi kuwahamisha maeneo hayo kutokana
na kupata adha ya mafuriko ya mara kwa mara, lakini hadi sasa
utekelezaji huo haujafanyika.
“Serikali ilituahidi kutupatia maeneo kule Kisesa, lakini tangu
wazungumze hadi sasa mwaka umepita hawajatuonyesha maeneo
hayo. Tunaiomba Serikali ifanye kila liwezekanalo ituhamishe
katika eneo hili tunusuru maisha yetu,” alisema Misanga.
Akizungumza kwa simu, mtendaji wa Kata ya Mbungani, Baruani
Hawadhi alisema maafa hayo siyo makubwa kwa kuwa hajapata
taarifa za vifo vya watu zaidi ya uharibifu wa mali za watu.
No comments:
Post a Comment