Pages

Tuesday, December 22, 2015

Mh Ummy Mwalimu aja na Kauli Mbiu Mpya ya Wizara kwa Wazee

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mh Ummy Mwalimu katika Muendelezo wa Kazi na Majukumu wa Uwazi wake, Lakini katika kutekeleza kauli mbiu ya Hapa kazi tu, ambayo Tangu Mh Rais John Pombe Magufuli kuchaguliwa na Watanzania na baada ya kuapishwa nakuanza kazi, Dunia Nzima kumekuwa na Habari na Breaking News kuhusu Rais wa Tanzania na Mawaziriwake.

Basi Kwa Hiyo Mh Waziri wa Afya Ummy Mwalimu juzi alivamia hospitali ya Bombo Tanga akaagiza Malipo yafanywe kwa Mashine za TRA ili kukusanya mapato.

Lakini sasa Mh Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya serikali  vya kutolea huduma za afya nchini, kwenye dirisha la mapokezi,vyumba vya madaktari na sehemu ya dawa zinaandikwe.
""MPISHE MZEE KWANZA APATE HUDUMA".
Agizo hili linakwenda   sambaba na uwepo wa madirisha ya wazee katika vituo vyote vya serikali vya kutolea huduma za afya.

Mhe Ummy pia amehidi kupeleka Bungeni Mswada wa Sheria ya Taifa ya Wazee ktk Bunge la mwezi Septemba ili kuhakikisha haki na stahili za wazee nchini zinatekelezwa kikamilifu. Wazee walieleza kero zao kubwa ni kupata matibabu, kutokuwa na kipato cha uhakika na vitendo vya kudharauliwa na jamii..

Tangu achaguliwa kuwa Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu hajapumzika wala kusema alale zaidi ya Masaa 5 amekuwa ni Waziri Mwanamke anaekwenda kwa Kasi na Speed Kubwa ya Kazi na Ufatiliaji wa hali ya Juu.

Waziri wa Afya alizungumza na Wazee wa Tanga jana wakiwakilisha Maoni na Matamanio yayo pia kero zao wakiwawakilisha Wazee wa Tanzania kwa ujumla, Ndipo Mh waziri akatoa Agizo la Hospitali zote za Nchi kuwa na Kipaumbele cha Wazee kwa kupata huduma zote pindi wafikapo Hospitalini.

Mh waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliyasema hayo Jana Tarehe 21 Dec 2015 Huko Mkoani Tanga.

"Mpishe mzee kwanza apate huduma"

No comments:

Post a Comment