TAARIFA KWA UMMA
UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA NA MGONGANO WA KIMASLAHI
wizara ya Afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto inayo jukumu la kusimamia Utoaji wa huduma za afya nchini kwa kuzingatia sera ya Afya 2007 na mkakati wa tatu wa sekta ya afya. Aidha ninatambua kuwa serikali iliridhia watumishi wa sekta ya afya kumiliki vituo vya afya pamoja na maduka
Ni dhahiri kuwa, umiliki huu wa watumishi wa Umma unaleta hisia hasi kwa wananchi kwa kuwa misingi ya mgongano wa maslahi, MH rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amekuwa akizungumzia suala hili katika nyakati tofauti hususani kukosekana kwa dawa katika vituo vya afya vya umma wakati vituo binafsi dawa zinapatinana wakati wote.
Vile vile kufuatiwa ziara zetu za kukagua utoaji huduma za afya katika maeneo mbali mbali, suala hili la upungufu wa dawa limeendelea kujitokeza kwa karibu zaidi. Baadhi ya wagonjwa walieleza kwa uchungu jinsi wanavyopata tabu ya kupata dawa hata zile ambazo wanatakiwa kupata kwa be nafuu ama zinazotakiwa kutolewa bure na serikali.
Kwa kuzingatia suala hili la mgongano wa maslahi, manung'uniko Mengi kutoka kwa wapokea huduma, hususani katika taasisi yetu ya saratani ocean road nimechukua hatua ya kumsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya saratani ocean road Dkt Diwani msemo ili kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine kubaini iwapo mgongano wa maslahi umeathiri utendaji wa taasisi ili iteuwe mtu ambaye atakaimu nafasi ya Mkurugenzi mtendaji wa taasisi mara moja
Kwa msingi huo wa uwazi na uwajibikaji ninawaagiza watendaji wote wa Serikali katika sekta ya afya hususani wakuu wa vituo vya kutolea huduma ya Afya wafamasia, Wauguzi, na waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma vya afya kukikiri kwa maandishi kwa ngazi zao za uwajibikaji endapo wanamiliki hospitali, zahanati, kliniki na maduka ya dawa ndani ya siku 21 kuanzia tarehe ya agizo hili
Ni Matumaini yangu kuwa, hili litasaidia kuziba mianya ya upotevu wa dawa, vifaa vya tiba katika vituo vya umma
Agizo hili halimuondolei wajibu kiongozi yeyote wa Serikali ambae anapaswa kujaza. Tamko la viongozi wa Umma kuhusu rasilimali na madeni kwa mujibu wa kifungu cha 9 na 11 cha sheria ya maadili ya kiongozi wa Umma na. 13 ya mwaka 1995 na 5/2001
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsi, wazee na watoto
23.12.2015
No comments:
Post a Comment