Na.Catherine Sungura-WAMJW
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto UMMY MWALIMU, ameitaka bodi na watendaji wa benki ya wanawake Tanzania TWB, kuhakikisha kuwa inawawezesha wanawake kiuchumi kwa kufikisha huduma hiyo mbali zaidi ili kuifanya benki kuwa kimbilio la wanawake kweli.
Akizungumza katika ziara yake ya mafunzo katika benki hiyo akifuatana na Naibu wake waziri Dakta HAMISI KIGWANGA, Katibu mkuu na watendaji wa Wizara hiyo UMMY alisema wanawake wa Tanzania wanajitoa sana katika kulea familia hivyo wakiwezeshwa watakuwa wamewezesha familia, vijana na Taifa kwa ujumla.
UMMY amesema watendaji wa benki hiyo ya wanapaswa kuweka utaratibu mzuri wa utoaji wa huduma ambazo zitaweka fikra za wanawake pale wanapotaka kuchukua mikopo au kuweka fedha zao katika benki kufikiria kwanza benki ya TWB.
“Mimi huwa naona uwezeshaj wa kweli wa wanawake ni kuhakikisha kuwa tunawawezesha kiuchumi na kielemu kwasababu mwanamke atashiriki kulima kupanda lakini ikifika kuvuna tu mazao sio yake hivyo endapo tutapata fedha zinazohusu mfuko wa wanawake serikalini tutaomba zipitishwe kwenye benki ya wanawake na tutakwenda kila Halmashauri kuanzisha saccos za wanawake ili waweze kupata fedha za kukopeshwa na benki ya wanawake,’’alisema UMMY.
Kwa upande wake Niabu Waziri wa Wizara hiyo Dakta HAMISI KIGWANGALA amesema benki nyingi zilizopo hapa nchini hivi sasa hazimilikiwi na serikali hivyo TWB inapaswa kuhakikisha kuwa inaweka mipango yake sawa ili iweze kubaki serikalini kwani lengo la kuanzishwa kwa benki hiyo ni kuleta ukombozi wa kiuchumi wa wakinamama kwani mama ni mlezi mkubwa wa familia.
Awalia Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo MOHAMED NYAMISAMA amesema tangu benki hiyo inakabiliwa na ukosefu wa umiliki wa jengo ambapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 wamelipa kodi ya pango shilingi bilioni mbili ambapo kila mwaka hulipa shilingi milioni 500 mia tano.
NYAMISAMA amesema pamoja na changamoto hiyo ya kodi kubwa ya pango benki hiyo imefanikiwa kukuza mtaji wake kutoka shilingi bilioni mbili nukta nane hadi shilingi bilioni nane nukta tano ikiwa na wanahisa 164 huku mwanahisa mkuu akiwa msajili wa hazina ambaye anamiliki asilimi 99 ya hisa.
Amebainisha kuwa hivi sasa inawateja elfu 56, asilimia 77 wakiwa wanawake na asilimia 23 wakiwa wanaume na wateja wa kampuni wakiwa asilimia tatu.
NYAMISAMA amesema benki hiyo ina matawi mawili Mkwepu na Kariakoo vituo vya huduma sita Dodoma, Mwanza, Njombe, Ruvuma na Iringa.
Naye Mkurugenzi wa benki hiyo MAGRET CHACHA ameimba serikali kuwasaidia kupata fedha maalum ili waweze kukopesha wanawake wengi Zaidi kwani kwa hivi sasa TWB inauwezo wa kukusanya shilingi bilioni saba kila mwaka.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment