Home » , » Waziri UMMY MWALIMU, ameitaka bodi ya Benki ya wanawake Tanzania TWB, kuwawezesha wanawake kiuchumi

Waziri UMMY MWALIMU, ameitaka bodi ya Benki ya wanawake Tanzania TWB, kuwawezesha wanawake kiuchumi

Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, January 16, 2016 | 7:51 PM

Na.Catherine Sungura-WAMJW

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto UMMY MWALIMU, ameitaka bodi na watendaji wa benki ya wanawake Tanzania TWB, kuhakikisha kuwa inawawezesha wanawake kiuchumi kwa kufikisha huduma hiyo mbali zaidi ili kuifanya benki kuwa kimbilio la wanawake kweli.
Akizungumza katika ziara yake ya mafunzo katika benki hiyo akifuatana na Naibu wake waziri Dakta HAMISI KIGWANGA, Katibu mkuu na watendaji wa Wizara hiyo UMMY alisema wanawake wa Tanzania wanajitoa sana katika kulea familia hivyo wakiwezeshwa watakuwa wamewezesha familia, vijana na Taifa kwa ujumla.
UMMY amesema watendaji wa benki hiyo ya wanapaswa kuweka utaratibu mzuri wa utoaji wa huduma ambazo zitaweka fikra za wanawake pale wanapotaka kuchukua mikopo au kuweka fedha zao katika benki kufikiria kwanza benki ya TWB.
“Mimi huwa naona uwezeshaj wa kweli wa wanawake ni kuhakikisha kuwa tunawawezesha kiuchumi na kielemu kwasababu mwanamke atashiriki kulima kupanda lakini ikifika kuvuna tu mazao sio yake hivyo endapo tutapata fedha zinazohusu mfuko wa wanawake serikalini tutaomba zipitishwe kwenye benki ya wanawake na tutakwenda kila Halmashauri kuanzisha saccos za wanawake ili waweze kupata fedha za kukopeshwa na benki ya wanawake,’’alisema UMMY.
Kwa upande wake Niabu Waziri wa Wizara hiyo Dakta HAMISI KIGWANGALA amesema benki nyingi zilizopo hapa nchini hivi sasa hazimilikiwi na serikali hivyo TWB inapaswa kuhakikisha kuwa inaweka mipango yake sawa ili iweze kubaki serikalini kwani lengo la kuanzishwa kwa benki hiyo ni kuleta ukombozi wa kiuchumi wa wakinamama kwani mama ni mlezi mkubwa wa familia.
Awalia Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo MOHAMED NYAMISAMA amesema tangu benki hiyo inakabiliwa na ukosefu wa umiliki wa jengo ambapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 wamelipa kodi ya pango shilingi bilioni mbili ambapo kila mwaka hulipa shilingi milioni 500 mia tano.
NYAMISAMA amesema pamoja na changamoto hiyo ya kodi kubwa ya pango benki hiyo imefanikiwa kukuza mtaji wake kutoka shilingi bilioni mbili nukta nane hadi shilingi bilioni nane nukta tano ikiwa na wanahisa 164 huku mwanahisa mkuu akiwa msajili wa hazina ambaye anamiliki asilimi 99 ya hisa.
Amebainisha kuwa hivi sasa inawateja elfu 56, asilimia 77 wakiwa wanawake na asilimia 23 wakiwa wanaume na wateja wa kampuni wakiwa asilimia tatu.
NYAMISAMA amesema benki hiyo ina matawi mawili Mkwepu na Kariakoo vituo vya huduma sita Dodoma, Mwanza, Njombe, Ruvuma na Iringa.
Naye Mkurugenzi wa benki hiyo MAGRET CHACHA ameimba serikali kuwasaidia kupata fedha maalum ili waweze kukopesha wanawake wengi Zaidi kwani kwa hivi sasa TWB inauwezo wa kukusanya shilingi bilioni saba kila mwaka.
MWISHO.

Picha ya pamoja kati Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla pamoja na uongozi wa Benki ya Wanawake Tanzania.
(Picha na Magreth Kinabo- Maelezo) 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati akifafanua jambo kuhusu kipaumbele cha Serikali cha kuwawezesha wanawake kiuchumi na kielimu ili waweze kupata kipato cha kuendesha familia zao wakati alipotembelea leo Benkji ya Wanawake Tanzania. Kushoto ni  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla.


Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wanawake  Tanzania , Mohamed Nyasana akitoa maelezo kuhusu  utendaji kazi wa benki hiyo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Naibu wa wizara hiyo Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla mara baada ya viongozi hao kuitembelea benki hiyo leo jijini Dar es Salaam, ambapo waliutaka uongozi wa benki hiyo kuwa wabunifu ili iweze kuwafikia wannachi wengi hususan waliokatika mazingira magumu.


Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla(kushoto)akifafanua jambo kuhusu Benki ya Wanawake Tanzania kuongeza mtaji ili kufikia walengwa wengi.Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati akifafanua jambo kuhusu kipaumbele cha Serikali cha kuwawezesha wanawake kiuchumi na kielimu ili waweze kupata kipato cha kuendesha familia zao, wakati alipotembelea leo Benkji ya Wanawake Tanzania. Kushoto ni  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wanawake  Tanzania, Mohamed Nyasana
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger