Kwanini Jakaya Kikwete Aheshimiwe.
Ndugu zangu.Jakaya Mrisho kikwete alikua ni amiri jeshi Mkuu na mwenyekiti wa CCM kwa miaka 10.
Mzee huyu ambaye mimi nimheshimu sana anapaswa kuheshimiwa na serikali ya sasa na watanzania wote, sina maana kwamba serikali ya sasa haimheshimu bali kuna watu wanadhani Mageuzi ya sasa ni kumkomoa Jakaya.
Jakaya angeamua kama Rais na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi kutumia mabavu na nguvu za vyombo vyake yoyote aliyemtaka angekua Rais.
Ni upuuzi uliovuka mipaka kwa namna yeyote kumpuuza mzee huyu Muungwana na mzalendo wa taifa hili.Wanaojaribu kumtukana Jakaya watayafanya haya pale Magufuli atakapo maliza kazi. Watanzania na hasa wana CCM, tumpongeze Rais Aliyepo anafanya kazi kubwa na nzuri bila kumdhihaki Jakaya. Ninayasema haya kwa sababu nimefanya kazi na Rais huyu,ninaujua uzalendo wake kwa nchi hii na uungwana wake wakujishusha.
Jakaya amelifanyia taifa hili mambo makubwa ikiwemo kutupatia Magufuli. wengi tunasema na kukejeli wana CCM na watanzania tujue Jakaya angeamua Kwa kiburi cha Madaraka kumrithisha amtakaye asingeshindwa hata tone kwa jinsi mfumo wa nchi ulivyo.
Magufuli ni zao la Hekima ya Jakaya
Tuache kumwandama Mzalendo huyu.
Kingu Elibariki
MP Singida West
No comments:
Post a Comment