KANISA LA EAGT KIBAIGWA LAFANYA HARAMBEE KWA AJILI YA WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI BUKOBA.
Kongwa,
Jioni ya Leo kanisa la EAGT Kibaigwa Wilayani Kongwa wamefanya Harambee yakuchangia Wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea Bukoba, Tetemeko ambalo limepelekea kupoteza uhai wa watu zaidi ya 17 na wengine kujeruhiwa na kupoteza Makazi yao pia kuharibu mali zao.
Harambee hiyo imefanyika Jioni ya Leo nakufanikiwa kukusanya Laki Mbili na Elfu Tano (205,000/=)
Harambee hii iliongozwa na Mchungaji wa Kanisa hilo Ndugu Aset Mwamezi ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kongwa (DAS) Ndg Frolensi Mushi, ambae alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deogratius Ndejembi, ambae alikuwa na makujumu mengine ya Kitaifa.
Akizungumza na Waumini hao Katibu Tawala amewashukuru nakuwasisitiza kuendelea na Moyo huo huo wakujitolea!
Shughuli hiyo imehudhuliwa pia na Diwani wa Kata ya Kibaigwa Mh Kapinye, Wazee wa Kanisa na Waumini wa EAGT.
No comments:
Post a Comment