Dodoma,
Ni Wiki kadhaa sasa zimepita tangu Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deogratius Ndejembi alipoamua Kuwasimamisha Kufanya kazi nakuwakamata Wenyeviti wa Madalali na Cargo Porters kwa Mahojiano zaidi ya Fedha walizokuwa wakikusanya wamepekeka wapi.
Apo awali Madalali hawa walikuwa wanatoza Tozo kwa Wakulima, Getini sokoni na Kila Tani ya Mzigo unaoingia Sokoni hapo walikuwa wanachukua Tozo. Mkuu wa Wilaya aligundua ufisadi huo nakupiga marufuku biashara hiyo.
DC Ndejembi Leo Ametamka Rasmi kuwafungulia Kifungoni ili waendelee na Biashara yao Madalali hao, baada ya kupata ufumbuzi wa namna gani sasa wanaweza kuendelea kufanya kazi yao ya udalali bila kuathili mapato ya soko. Mbali na hilo kawaamuru wajisajili ili wawe na chama kinachoeleweka na watambulike kwa Majina na Vitambulisho vyao wavae Muda wote wanapokuwa kazini kwao.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Kongwa amewapa Ofa ya Kufanya Kazi yao ya Udalali Bure hadi Mwezi wa Kumi ambapo sasa watakuwa wanalipa Kodi kwa Bodi ya Soko.
Madalali hao kwa sasa ni Marufuku kutoza tozo zozote ndani ya soko hilo kama walivyokuwa wakifanya awali kwa kutoza Getini, Kwa wakulima, Kila Tani nk... Jambo ambalo lilikuwa ni kinyume na Taratibu na Sheria za ukusanyaji Kodi. Kwa sasa Tozo hizo zitatozwa na Bodi ya Soko tu!
Mkuu wa Wilaya amewaomba Pia Madalali hao kwa Kuchapa kazi kwao nakujipatia Mapatao Bali wachangie Madawati.
Swala hilo Madalali wamelipokea kwa mikono miwili na wameahidi kuchangia Dawati 20 mwezi ujao na Cargo Porters pia wameahidi Dawati 10.
Wilaya ya Kongwa inaupungufu wa Madawati zaidi ya Mia Tano (500).
Lakini Pia akizungumza na Madalali hao mbele ya DC Ndejembi Mh Diwani wa Kata ya Kibaigwa amewaomba Madalali hao kuwa Wachapa kazi kwani wamepata DC mwenye kujali Maendeleo nakusikiliza Kero za Wanachi kwa Wakati ivo Hata Swala la Madawati Kawaomba watoe Dawati Kumi kisha Baada ya Mwezi watoe zingine Kumi ivo Wakawa wameahidi Dawati ishirini (20) kwa awamu.
Pia akizungumza na DC Mkuu wa Kituo cha Police Kibaigwa amemuhakikishia Ulinzi wa hali ya Juu Sokoni hapo na Kibaigwa kwa ujumla.
DC Ndejembi akikagua maeneo ya Soko hilo akiwa na katibu wa soko kuu la Kimataifa la Kibaigwa
DC Ndejembi akizungumza na Madalali eneo la soko Kushoto kwake ni Diwani wa Kibaigwa alipofika na akawa akipewa maelekezo mbele ya madalali hao
Madalali hao wakisikiliza kwa makini
No comments:
Post a Comment