Taarifa zilizonifikia ni kwamba Kiongozi wa Mgomo wa Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka ametekwa na ameokotwa akiwa katika hali mbaya sana.
Kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forums, Dk Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye 'face to face' kwa ajili ya mazungumzo.
Tukio hilo limetokea wakati kumekuwepo na mgomo wa madaktari nchi nzima ambao hata hivyo wameonekana kusalitiana kwa kutokuwa na msimamo wa pamoja, kwani maeneo mengine huduma zimeendelea kama kawaida.
Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.
Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------
Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.
Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.
Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.
Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.
UNA MTAZAMO GANI JUU YA HABARI HII? NiPE MAONI YAKO
Post a Comment