Test Footer

Habari Mpya
Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

WARAKA No. 2 WA MHE. SPIKA KUHUSU UGONJWA WA CORONA

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, March 17, 2020 | 1:33 AM




Peter Msigwa alipiwa na Rais Magufuli.

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, March 12, 2020 | 5:35 AM

Rais John Magufulileo Tarehe 12/03/2020 amemlipia Sh38 milioni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa kati ya Sh40 milioni alizotakiwa kulipa faini baada ya kuhukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, July 10, 2018 | 7:08 AM

*MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE KATIKA JIMBO LA DODOMA MJINI*

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde* leo amepokea mifuko ya Saruji 724 yenye thamani ya *Tsh 10,000,000* kutoka *Benki ya CRDB* kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa,Nyumba za Walimu na matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Dodoma Mjini.

Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji,Mkurugenzi CRDB Tawi la Dodoma *Bi Rehema Hamis* amesema kwamba Benki ya CRDB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano chini ya *Mh Rais Dr John Pombe Magufuli* na uchapakazi wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde katika kuboresha miundombinu ya Elimu.

Akipokea mifuko hiyo ya saruji,Mbunge Mavunde ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo ambao utalenga kupunguza changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa 1035 katika Jimbo la Dodoma Mjini ambapo kwa hivi sasa anaendesha kampeni maalum ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi na kwa kuanzia mfuko wa Jimbo umetoa matofali 32,000 na mifuko ya Saruji 2,560 kwa kata mbalimbali.

MAVUNDE AWATAKA WADAU WA MICHEZO DODOMA KUSHIRIKIANA KURUDISHA HESHIMA YA DODOMA KATIKA MPIRA WA MIGUU

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, June 3, 2018 | 11:18 PM

*MAVUNDE AWATAKA WADAU WA MICHEZO DODOMA KUSHIRIKIANA KURUDISHA HESHIMA YA DODOMA KATIKA MPIRA WA MIGUU*

Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka wadau wa Mpira wa Miguu katika mkoa wa Dodoma kushirikiana na kuweka nguvu ya pamoja ili kurudisha heshima ya Mkoa wa Dodoma katika mpira wa Miguu nchini kwa kuwa na Timu ya Ligi kuu na kuongeza hamasa kupitia mashindano ya ligi mbalimbali ili kuibua vipaji.

Mavunde ameyasema hayo leo katika kijiji cha Msanga,Wilaya cha Chamwino -Dodoma wakati akifungua mashindano ya Kombe la *Kisalazo 2018* ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ndg Juma Kisalazo na Mbunge wa Jimbo la Chilonwa Mh Joel Makanyaga Mwaka.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christine Mndeme , leo tarehe 3/6/2018 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru Na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Christopher Ole Sendeka.

*RUVUMA NA MWENGE WA UHURU* 


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma *Mhe Christine Mndeme* , leo tarehe 3/6/2018 amekabidhiwa *Mwenge* wa Uhuru Na Mkuu wa Mkoa wa Njombe *Mhe Christopher Ole Sendeka* .


Mwenge wa *Uhuru,* ukiwa Mkoani *Ruvuma* unatarajia kuzindua Jumla ya *miradi 70* yenye thamani zaidi ya Shilingi *bilioni 11.* itafunguliwa,kutembelewa na  kuwekwa mawe msingi.


Mwenge wa *Uhuru* utakimbizwa Halmashauri Nane za Mkoa wa Ruvuma.


 *Mwenge wa Uhuru kwa Maendeleo CHANYA ya Mkoa wa Ruvuma !*

KIFO CHA AKWILINA NI MTAJI WA SIASA KWA WANASIASA UCHWALA WA TANZANIA.

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, February 20, 2018 | 2:12 AM

KIFO CHA AKWILINA NI MTAJI WA SIASA KWA WANASIASA UCHWALA WA TANZANIA.

Nazidi kusikitishwa na Kuumizwa kwa Kauli na Matendo ya wana Siasa Uchwala wa Tanzania.
Tangu Binti Mrembo na mpole mwenye kila aina ya Sifa alizokuwa nazo enzi za uhai wake, Kabla ya Kupoteza Uhai wake Kwenye Ghasia za Tamaa za madaraka za Wanasiasa waliofanya Maandamano yasio na kibali huko Kinondoni. Bado wana siasa hao hawajaridhika wanaendelea kusema na kufanya Msiba wa Akwilina kama Mtaji wa Siasa zao za Maji Taka hapa Nchini Tanzania.

Haijawa mara ya Kwanza kwa CHADEMA Kufanya maandamano bila Kibali wala Taarifa makusudi na kila wafanyapo hivyo basi Kifo au Vifo hutokea bila kusahau Majeruhi, wizi ama uharibifu wa mali za Raia hutokea na baada ya hapo! Hoja ya Msingi huwa ni Picha za Kifo na Majeruhi kupigwa nakuanza kusambazwa kama mtaji kwao na kwa maboss wao wa Nje na Ndani ya Nchi.

Ndugu yangu kadili unavyoendelea Kusoma Ujumbe huu naomba nikuulize!
Kwani kama CHADEMA wasingefanya maandamano Kifo cha AKWILINA KINGEKUWEPO LEO HII?

Kama kweli CHADEMA ni waadilifu na wapenda Taratibu, Sheria, Kanuni na Haki kwanini hawakutaka kufuata taratibu za Madai yao kwa Kuongozwa na HEKIMA na BUSARA kwa Kufuata taratibu za maandamano ama Barua za kiofisi kudai hizo haki zao? Ama kutuma watu wachache kufuatilia hizo Hati za Viapo?

Sasa Tizama Akwilina hakuwa kati ya Waandamanaji bali alikuwa Mpita Njia tu akienda kupambana kutafuta ama kuijenga Future yake. Kaja mwana kaifyatua na ikamtoa Uhai Binti na Kukatisha Ndoto zake zote na za FAMILIA YAKE NA TAIFA KWA UJUMLA kwa KUPOTEZA NGUVU KAZI YA TAIFA.

Leo AKWILINA KAWA MTAJI WA SIASA hasa apale unapoona wanasiasa Kila siku wanakuja na hoja za Waziri wa Ulinzi, Kamanda wa Kanda Maalumu, Mkurugenzi nk… Wajiuzuru Kisiasa kwa kosa la Wachache kuamua kufanya Maandamano tena wakijua wakifanya hivyo Mauwaji na majeruhi lazima watakuwapo, Na kuthibitisha hilo Rejea Kauli za Mikutanoni, Kauli za Vingozi walipokuwa tume ya uchaguzi siku mbili kabla ya uchaguzi wametamka sana Mauwaji Kutokea Nk… Utaona kifo cha AKWIlINA kimekuwa sio Msiba tena bali ni mtaji wa Wanasiasa na Hujipanga kufanya hivyo ili Kutafuta HURUMA ZA DAMU ZA WATU AMBAO HUPOTEZA UHAI KWA GHASIA AMBAZO HUSABABIUSHWA NA HAWA WENZETU WA CHADEMA, iFIKE mahala Watanzania Tujue Mbinu hizi na Tukemee kwa Pamoja.

Ningefurahi sana kama Tusingekuwa na HOJA YA KUWAJIBISHANA KISIASA BADALA YAKE TUSHIRIKIANE KUMTAFUTA ALOFANYA TUKIO HILO HASAA…!  IWE NI ASKARI AMA RAIA ALOKUWA NA BUNDUKI AMA KIONGOZI MIONGONI MWA WALOKUWA WAKIANDAMANA ili Huyo kwanza apate Stahiki yake yakufanya kosa la mauwaji kwa Makusudi ama kwa Bila kukusudia. Na iwe Fundisho kwa Wakati Mwingine.

Manake Tusikimbilie Kuwajibishana kisiasa nakuacha Mzizi wenyewe!
Tukumbuke Risasi Ilipigwa na mtu kwa Utashi wake akijua anaenda kujeruhi ama kuuwa, Basi apatikane na tujue alitumwa na nani, Sio kukaa nakuwasingizia Viongozi wa Jeshi la Police na CCM.
Lakini pia Tusisahau kuwa Kuna uwezekano kuwa Risasi ile Ilikuwa ni Bahati  mbaya kwa alokuwa na Bunduki husika kumfyatuka ama kufyatua akiwa hana matarajio itaenda kupiga kwenye Gari nakusababisha Kifo cha Binti AKWILINA.

Na hata kama ni Askari naomba ifahamike kuwa Kuvaa kwake unifomu ya Jeshi la POLICE Haimfanyi kosa lake kuwa kosa la Askari ni kosa lake tu yeye mwenye Mtu Binafsi na Hata maakamani atapanda mwenyewe na mashitaka atayajibu yeye na sio Jeshi la police, na itakuwa hivyo kama ni Raia ndio kafanya hivyo pia.

Wewe Unaesema kuwa huu ni mpango wa CCM na Police, Jiulize Mtoto AKWILINA ameikoasea Nini CCM au Jeshi la Police Mpaka iamuriwe auwawe? Na Tangu lini CCM na Police wakawa Wajamaa nakushirikianankufanya mauwaji? Think Twice tusichume dhambi za Buree…!

Watanzanzia Tumekuwa tunajipa majibu na Hukumu ambazo hatupaswi kujipa kabla ya kujua kweli, na Hatuwezi kwenda mbele kwa amani kama tunataka kuishi kwa hisia.

WANASIASA ni watu Wabaya sana Wanaweza Lijenga ama kulibomoa Taifa kwa Tamaa zao na subira zao,  Kila Chama ambacho kiko Nje ya madaraka Huhitaji kuingia madarakani kwa Namna yoyote ile, iwe kwa UONGO, WIZI WA KURA, UHASI, MAPINDUZI Nk…. Ivyo Wanasiasa  wako tayari kwa lolote ili wao wapate nafasi serikalini au uongozi serikali, wenyewe husema Kumiliki Dola

Utaona Kauli za CDM zakupoteza uhai wa watu kwenye maandamano na mikutano kwao sio issue sana ila issue  ni ushindi wao tu! Ama kutimiza jambo husika.
Kinachofanyika na hawa wana CDM ni Kujenga Chuki kwa Raia ili walichukie Jeshi la POLICE , Wawachukie watanzania wenzao ambao wanaamini kwa CCM,

Baada ya Kifo cha Binti Akwilina utaona kaulI nyingi sana za kichochezi zinaendelea kwenye Midomo ya Wanasiasa hawa, Kauli hizi zinakuwa ni marudio ya kauli zao za awali ambazo walizisema mapema kabisa walipokuwa katika kampeni kuwa Watu watakufa na kujeruhiwa, hii inatupa majibu na hisia kuwa wamejipanga na walijipanga kufanya ama kusababisha haya kwa faida zao za kisiasa.

Je! UNAJUA KUWA KUNA ASKARI WALIPIGWA MAPEMA KABISA KBLA YAKUANZA KUWATAWANYA NA ASKARI HAO WAMELAZWA KWA MAJERAHA NA MAUMIVU MAKALI YA KICHAPO CHA WAANDAMANAJI CHINI YA USIMAMIZI WA VIONGOZI WAO?

MWISHO. Niwaombe wanasiasa wa Tanzania kuwa waungwana walau kwa baadhi ya mambo, Najua Tamaa za Uwongozi zinawasumbua sana lakini kumbukeni Nafsi za wanaopoteza uhai zinasononeka sana, na Kusema uwongo ama kusingizia Jeshi la Porisi ama kurushiana mipira kuwa ni CDM ama ni CCM haitasaidia sana mwisho wa siku sisi wote ni mavumbi na Mavumbini tutarudi na Siku nya hukumu itafika na kila mmoja atapata stahiki yake.
Tamaa za Uwongozi zisituondolee utu wetu.
Kifo cha Akwilina kisifanywe Mtaji wa Siasa, Msibani kuleta Unafiki ni dhambi kubwa sana.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AKWILINA MAHARA PEMA PEPONI! AMINA…….!!

Peter L. Dafi

MTETEZI WA WANYONGE

Mbunge Ridhiwani Kikwete Amegawa Vifaa vya Kuchezea Mpira kwa Team ya Jimbo la Chalinze

Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, August 11, 2017 | 2:12 PM

Mbunge wa Chalinze leo amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo la chalinze zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya bagamoyo.

Sherehe hizo zilizofanyika kimange zilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Madiwani wote wa Jimbo la Chalinze na watendaji wao wa kata ambao walipokea jezi kwa niaba ya timu zao. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya  ambaye ndiye muandaaji mkuu wa mashindano hayo akishirikiana na wabunge wa majimbo yote

Pamoja na kugawa jezi , mbunge wa chalinze aliwaahidi kuwapatia mshindi wa pili wa mashindano Pilkipiki ya Miguu miwili, na jezi kwa timu zote Tatu za juu kufuatia mkuu wa wilaya kuwachangia mshindi wa kwanza pikipiki ya Toyo ya miguu mitatu ili itumike kwa shughuli za kipato kwa vijana.

MAISHA YA MAZOEA CCM IFIKIE KIKOMO ~ HAPA KAZI TU!

Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, July 9, 2016 | 11:23 AM

MAISHA YA MAZOEA CCM IFIKIE KIKOMO ~ HAPA KAZI TU!

Nasema hivi.....!

Hakuna Kipindi ambacho wana CCM wanatakiwa kuwa Makini na siasa kama Kipindi hiki.

Hakuna Kipindi wana CCM wanatakiwa Kuacha Tabia zakimazoea km kipindi hiki.

Hakuna Kipindi ambacho chama na jumuiya zake kinapaswa kuajiri Vijana na Watu wenye Uwezo Mkubwa wakufikiria nakupanga mikakati ya Kisasa inayokwenda na Wakati kama Kipindi hiki.

Tunaposema vijana.... Umri siyo tija ingawa ni Jambo la maana kwa Mustakabali wa taifa na Chama.... Bali tunahitaji vijana wanaoweza kuunganisha kasi yao ya mwendo huku wakitumia busara na hekima wanazochota kutoka kwa wazee na waasisi wetu.... Sifa siyo Umri, Sifa iwe ni uwezo wa kutenda na kufanya, kuona na kuangalia, kusikia na kusikiliza na kufanya kuyafanyia kazi yote kwa pamoja...... Huyo ndiye kijana apewe nafasi......

Hakuna Kipindi ambacho hatutakiwi kuishi kwa UWoga, Unafiki, Uzandiki km kipindi hiki, tunapaswa kuwa wawazi ili kujua tatizo liko wapi.

Tabia za kufanya Ziara nakufika Mikoani uko, Katibu anatoa Takwimu za Uwongo za uwingi wa Wanachama ama utendaji kazi zake wakati hazina ukweli na anahali ngumu na Tete yakisiasa ktk eneo lake ikome.

Tunapaswa kufanya Kazi kubwa ya Siasa kwa umakini ili Chama kiwe imara na Serikali iwe Imara na Hatimae Ilani ya CCM itimizwe kwani nilazima tuwe shupavu ili itekelezeke kwa 99% kwani CCM ndio Chama Tawala na CCM ndio yajenga Nchi.

Kwani Mafanikio na Mipango chanya itakayotekelezeka ndio haswaa itajenga mizizi imara itakayoifikisha CCM Miaka 50+ ijayo.

Swala la Uwanachama nilazima sasa tuhakikishe Wanachama wa CCM wanafanyiwa Vetting na Mafunzo yakikada kama huko awali ilivyokuwa lazima Mwanachama apitie mafunzo miezi 3 tujiridhishe kuwa kafuzu na yuko sawa ki Itikadi "NILAZIMA TUWE NA WANACHAMA WA ITIKADI NA SIO WANACHAMA WA KADI" hawa wanachama wa Kadi ndio wanaotuyumbisha leo CCM kesho NCCR na Tulimuamini tukampa cheo bila kujua Ulaji ndio ulimleta CCM.
Wakirudisha Kadi za Vyama CDM na Vyama Pinzani vingine Basi Tutawapokea kisha Watakaa kupewa Darasa la Itikadi kwa Miezi 3 ili Tujiridhishe kuwa Anania na amekwiva.

Pia nikuhakikisha tuna Team inayochunguza Mienendo ya Wanachama hawa na tena iwe Fear isije ikasema uwongo.

Tunahitaji Mabadiliko ya Kweli kama tulivyoimba Katika Kampeni.

Naamini Kuwa Tunapoelekea Kumkabidhi M/kiti Mpya Chama basi Haya yawe ni Vipaumbele pia vya Mambo yakushughulikiwa ndani ya Chama.

Naitwa Peter Dafi

Mtetezi wa Wanyonge.
09/07/2016

VILAZA WA UKAWA ACHENI USONGOMBWINGO

Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, July 8, 2016 | 8:33 AM

VILAZA WA UKAWA ACHENI USONGOMBWINGO
Uteuzi wa makatibu tawala wa wilaya umeibua taharuki..... Si taharuki kwa kuwa eti kweli ni taharuki bali kwa kuwa kuna VILAZA nchi hii wako taharuki na akili zao ni kutafuta shari kila siku....
Uteuzi wa watawala hawa umezingatia weledi, uadilifu umakini na dhana ya kutimiza malengo ya pamoja tukiwa wa moja.
Kilichoonyeshwa na magazeti mengi pamoja na maoni ya WAPIGA DOM wa UKAWA ni wivu unaitwa USONGOMBWINGO..... Ni wivu wa Joka la Kibisa...... Linazingira miti ya matunda na kula haliwezi...... Hii ni akili mbovu kabisa.....
Uteuzi huo umezingatia uwezo wa kutekeleza malengo ya pamoja kwa mlengo mmoja yaani GOAL CONCLUENCY kwa maana tumepata makatibu tawala wanaoimba wimbo mmoja na kuruka pamoja na kutua pamoja na Rais, waziri, RC, DC na wenye ilani yao Chama Cha Mapinduzi.....
This time hatujafunga mazee..... Yaani tumeondoa tatizo la rangi rangi sasa kama kuna mtu haridhiki afanye jambo moja tu.... Akasikilize nyimbo za Saida Karol atagundua kuwa yampasa AJINYONGE
Nitumie ukurasa huu kuwaasa, kuwaonya na kuwakanya wapotoshaji wote.... Kwamba tutafika ukomo wa kuwavumilia..... Sasa mumekosa hoja..... Badala ya mngekuja labda mseme walioteuliwa hawana weledi.... Mnakurupuka eti wameteuliwa Makada....... Kazi ya HAPA KAZI TU mlitaka wateuliwe JANJAWEED (Yaani wagonga viroba na Bangi)????? NO WAY......
Waandishi wa habari wachache mnaotumia kurasa za magazeti KUPOTOSHA mantiki na ukweli...... Tumieni kurasa hizo kuelewesha Umma...... Mbona inawezekana........
Wanasiasa UCHWARA nyie UKAWA kwenu sina hata la kuwaomba bali kuwaamrisha mkae kimya maana nyie blue kwenu ni nyeusi iliyofifia, Njano ni nyekundu ikiwa mbali mkiona nyeupe mnajua hamna kitu na nyeusi kwenu ni Usiku...... Please shut up......
Kama ilivyo haiwezekani kuteua baraza la mawaziri nje ya CCM, basi nje ya CCM huwezi kupata chochote....... Kama huko nyuma mlizoea kutuingizia MBU kwenye Net, this time imekula kwenu NET LIMETEMA MBU WOTE chezeni nao......
Kwa uhalisia subirini muone ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi itakavyotekelezwa alafu na nyie hatutawabagua kwenye maendeleo msijisikie vibaya mkiona shule, Hospitali, barabara, viwanda na huduma nyingine za Jamii, msije mkasusa maana akili yenu mnaijua wenyewe.... BANGI SANA
Naona Mshaanza kutokwa na mapovu baada ya uteuzi wa wakurugenzi, Mara Kakosea kawahamisha nani na nini Ufafanuzi ushatolewa kwa marekebisho hayo.
Acheni unazi bana
Na Mwaka HUU Mtaisoma Namba Kisawasawa......
........
MTANYOOKA TU.
HAPA KAZI TU!
By
Peter Dafi
Mtetezi wa Wanyonge.

Mkuu wa Wilaya Ally Salum Hapi Akabidhiwa Fimbo yakuchapia Mafisadi na Wazee wa IKICHE

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, May 8, 2016 | 3:09 AM

Mh DC wa Kinondoni Ally Salum Hapi awa mgeni Rasmi katika kikundi ambacho kina wanachama 76  kati yao hao Wanaume ni 36 na Wanawake ni 40.

IKICHE ni kikundi ambacho kinafanya shughuli za kukopeshana kwa Shida na Raha.
Kikundi kina Miaka Minane Leo hii na kimedhaminiwa Cheti cha Usajili, Kikundi cha IKICHE kilianzishwa 13/04/2008 Jijini Dar es salaam

Wanachama wa IKICHE
Wageni waalikwa wakiwemo Maafisa wa Bank ya DCB kwa ajili ya kuelimisha Maswala ya Mikopo na kuwapatia Mikopo.
Meza Kuu Mh Mkuu wa Wilaya Akiwa na Viongozi, Kushoto ni Kada wa Chama Ndg Nyang'anyi, anaefuata ni Ndg Malema Kisha M/Kiti wa Kikundi cha Ikiche Ndg Saidi Mafita Anafuata Mkuu wa Wilaya Mh Ally Hapi Na Mwisho ni Ndg Abby Kaungu.
Ndg Nyang'anyi, anaefuata ni Ndg Malema Kisha M/Kiti wa Kikundi cha Ikiche Ndg Saidi Mafita Anafuata Mkuu wa Wilaya Mh Ally Hapi Na Mwisho ni Ndg Abby Kaungu
Meza hii Kuna Kushoto ni Nobert Kobwino, Kisha Wanaofuata ni Wazee Walezi na Washauri wa Kikundi cha IKICHE.
WANACHAMA WAKIUME WA IKICHE
Wanachama wakinamama wa Kikundi cha IKICHE.

Baadhi ya Wakinamama wakisikiliza Kwa umakini.
Katibu wa Kikundi cha IKICHE Ndg Hashimu Ally akisoma Hotuba kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Mzee Mlezi wa Chama cha IKICHE amemkabidhi Ndg Ally Salum Hapi Kuwa Mlezi wa Kikundi cha IKICHE.
Mzee Kamkabidhi Bakora maalum kwa Kuchapia Wahujumu Uchumi na Mafisadi, Matapeli nk...  Wote wapatikanao Wilaya ya Kinondoni.
Pia Kakabidhiwa Bahasha yenye Nyaraka za Kibobezi.
Mh Ally Akimshukuru Mzee kwa Zawasi na majukumu aliyomkabidhi.


Mkuu wa Wilaya Akabidhi Cheti kwa Kikundi Cha IKICHE
Cheti cha Usajili wa Kikundi hicho
Picha ya Pamoja na Wazee waasisi na walezi wa Kikundi.
Picha ya pamoja na Viongozi wa Kikundi, Kushoto ni Muweka Azina, Mkuu wa Wilaya kisha Mwenyekiti wa Kikundi na Katibu wa Mwisho.
Picha ya Pamoja na Makada wa Chama cha Mapinduzi waliofika ktk Sherehe hiyo, Kushoto ni Malema, Kisha John Mboro, Mh DC Hapi, Peter Dafi, Abby Kaungu na Mwisho ni Ndg Nyang'anyi.
Hotuba ya Mh DC Hapi mbele ya Wana IKECHI
Picha ya Pamoja na Wamama wanakikundi cha IKECHI.
Picha ya Pamoja na Wanaume wanachama wa Kikundi
Picha ya Pamoja na Viongozi wa Chama cha IKECHI
HAPA UNAWEZA KUONA VEMA FIMBO ALOKABIDHIWA NA MZEE ALIEKUWA MLEZI.

DC HAPI ATEMBELEA GHAFLA HOSPITALI YA MWANANYAMALA USIKU LEO

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, May 4, 2016 | 2:52 PM

DC HAPI ATEMBELEA GHAFLA HOSPITALI YA MWANANYAMALA USIKU LEO
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo usiku ametembelea hospitali ya Mwananyamala kujionea utoaji wa huduma hasa wakati wa usiku.

Hapi ambaye alitinga hospitali hapo kama mgonjwa wa kawaida akivalia kofia ya mkeka alitembelea mapokezi, vyumba vya daktari na baadae kumshtukiza kiongozi wa madaktari kwa usiku huo ofisini kwake akimuelekeza kumtembeza sehemu mbalimbali za hospitali hiyo ambayo Mkuu wa wilaya alitaka kuziona.
Mh. Hapi alitembelea wodi ya watoto, wanaume, wodi ya kina mama, wodi ya dharura (emergency) na kumalizia chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) ambako alizungumza na wagonjwa, kuwajulia hali na kujionea changamoto zinazowakabili.
Akiwa chumba cha kuhifadhia maiti Mh. Hapi alifanya mazungumzo na mhifadhi maiti na kujua changamoto zinazoikabili ofisi yake.
Hospitali ya Mwananyamala inatajwa kuwa na changamoto nyingi za utoaji huduma hali inayosababisha malalamiko ya mara kwa mara ya wananchi.

Hapa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliingia nakujipanga ktk Dawati la wagonjwa wanaongoja kuingia Kwa Dr kusikilizwa!

Hatimae Wagonjwa walipungua na akabakia mama Mmoja ambae baada ya mama kuingia DC Hapi alifuata kuingia kwa Dr wa Zamu alokuwapo OPD.

Baada yakuzungunza na Dr Alimuelekeza nakujitambulisha Kuwa yeye ni Mkuu wa Wilaya na angependa kujua hali ya Huduma na wagonjwa ikoje!
Ivo aliomba kutembelea Wodi za wagonjwa kisha Msafara ukaanza kutembelea Wodi hizo.
DC alifika Wodi ya Wanaume nakujionea Changamoto za ukosefu wa Neti, Mashuka na Upungufu wa Vitanda kwa Baadhi ya Wodi.
DC Hapi alipotoka alikwenda Nje ya Hospitali nakununua Dawa, Kisha Kudai Risiti Jambo ambalo Lilizua Mtafaruku kwa Mama Muuza Duka, Mama alitoa maneno makali na yakejeli kwa Kumwambia DC Kuwa hana Risiti kama Hataki Alete Dawa amrudishie Pesa yake.
Ndipo DC alipobadilika nakumkalipia Mama Kabla hajajua Nani anazungumza nae akastuka na kutoa Risiti.


Pozi la DC Hapi akingoja Mama anaandika Risiti
Mama Muiza Duka la Dawa akiandika Risiti
Picha Hii inaonyeaha DC Hapi akiwa amesimama na Dr  aliekuwa akimtembeza na hapa ni Mlango wakuingia Mochwali Alikuta Magodolo yako pale na kuna Wagonjwa wanalala Chini ivo akahoji Vipi Magodolo yako pale na kuna watu wanahitaji.
Jibu likawa Yale yako matengenezoni kwa kuyawekea Makava.
DC Hapi akizungumza na Bwana Ally Mbwambo muudumu wa Chumba chakuhifadhia Maiti.
Alijielezea nakusema Chamoto ktk Kitengo chake kwa sasa ni Kuwa Jokofu moja limeharibika ivo wanatumia Dawa sana Kuhifandi Miili.
Lakini pia Chumba huwa kidogo kama Inatokea Ajali kwa wingi na Panapotokea Police Kesi ambazo Miili inakuwa haitike haraka ivo huihamisha nakupeleka Muimbili nk..
DC alimaliza Ziara yake yakustukiza kwa Kuwa kugundua Mapungifu ya NET, MASHUKA NA UPUNGIFU WA MADAKTARI, kwani Usiku hu Wahudumu kila Mahala ni mmoja mmoja itakuwajw kama Emergence itatokea.
Ivo DC amenote na anakwenda kushulkia kero na changamoto hizo.

TAMKO LA JUKWAA HURU LA WAZALENDO JUU YA MWENENDO WA BUNGE (JUHWATA)

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, April 24, 2016 | 2:04 AM



JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA-(JUHWATA)
TAMKO JUU YA MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE
Ndugu wanahabari poleni na majukumu ya kulihabarisha Taifa, ndugu wanahabari tulio mbele yenu ni wajumbe wa jukwaa huru la Wazalendo Tanzania ( JuhwaTa). Kama mnavyojua jukwaa huru la WAzalendo ni taasisi huru inashughulikia mambo mbalimbali ya kitaifa ikiwepo, Mijadala, Makongamano,Matamko na Elimu kwa umma kuhusiana na mambo mbalimbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi kwa maslahi mapana ya Taifa.
Leo tumewaita, Jukwaa likiwa na masikitiko makubwa kuhusu mwenendo wa shughuli za bunge, hususan bunge linaloendelea sasa pale Dodoma, bunge la bajeti, Kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inalitaja bunge kuwa ndio chombo kikuu ambacho kitakuwa na madaraka , kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya wabunge kususia mijadala,vikao na shughuli nyingine za bunge kwahiyo wamekuwa wakivunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 63 (2) na kutupelekea wananchi kukosa fursa ya uwakilishi kutoka wa wale tuliwachagua huku wao wakiendela kupata stahiki zao kwa maslahi yao. Kwa mfano, Watanzania tunatambua kwamba kuna baadhi ya wabunge walisusia bunge maalum la katiba matokeo yake wananchi tukakosa mawazo mbadala kutoka kwao na walioumia ni wananchi wanyonge na sio wao.
Jukwaa linasikitika sana, Mnamo 22/04/2016, Kambi Rasmi ya Upinzani  Bungeni, ilishindwa kuwasilisha Mapendekezo Mbadala wa Bajeti Ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni za bunge kwa visingizio vya kwamba serikali haina Mwongozo wa kuiongoza nchi, Serikali kubana sana Matumizi bila kuwashirikisha wao kama Wabunge na Hatua mbalimbali ambazo mh Rais John P Magufuli za  Kutumbua majibu hadharani bila kutoa mchakato  wa watumbuliwa wa ufisadi kujitetea kwanza. Wananchi tunaamini kabisa kuwa, Kambi Rasmi imeshindwa kuwasilisha na kutoka nje kwa sababu mosi, Mpango Uliowasilishwa Bungeni na serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mapendekezo ya Bajeti Ya Ofisi Ya Waziri Mkuu, umepokelewa vema na wananchi  na wasomi  huku wakiupongeza kwani Mpango umejikita katika, Ujenzi wa reli ya kati kwa standard gauge, Kuboresha Makusanyo ya Kodi, Vita Vya Ufisadi na Ubadhirifu, n.k. Pili Kambi Rasmi inawezekana kabisa hawakuwa na Hoja ya kupinga na njia pekee ni kutoka nje kuunga mkono Mapendekezo ya serikali.
Ndugu wanahabari ikumbukwe, Utaratibu, michakato na kuonea haya dhidi ya Mafisadi kimekuwa ni kilio cha wananchi wengi na tunashukuru mh Rais kusikia kilio chetu na kuweza kutufuta machozi yetu kwa vitendo. Pia ikumbukwe nchi hii imeliwa na Mafisadi kwa kuendekeza Michakato na Utaratibu, na sisi kama wananchi hatutakubali michakato na taratibu katika kushughulikia mafisadi wa Taifa iendelee. Na katika kumuunga mkono mh Rais, siku ya hotuba ya uzinduzi wa bunge la 11,Mh Rais alituomba Wananchi wazalendo tumuunge mkono katika vita aliyoianzisha ya kupambana na Mafisadi, Kubana matumizi, Kurudisha nidhamu ya Utumishi wa Umma, Uchapakazi na Uzalendo na sisi kama wananchi wanyonge tunauunga mkono jitihada hizo na tunamwambia na kumtia moyo kwamba tupo nyuma yake katika vita hii ijapokuwa wapo wachache wanaojaribu kuirudisha na kuhujumu jitahada zako kwa maslahi yao binafsi na Mafisadi wanaowatumia.
Ndugu wanahabari, sote tunajua mh Rais alipokuwa akiomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi alikuwa akitoa ahadi na viapombele mbalimbali na sasa mh rais amezidi kutekeleza ahadi zake kwa vitendo kwa wananchi aliowaahidi, mfano Kuwa na baraza dogo la Mawaziri, Elimu bure, Kubana Matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha zitakazo okolewa kwenda kutatua kero sugu za wananchi wake, kupambana na Mafisadi nk. Sasa tunashangaa kuwekuwepo na baadhi ya watu wakiwemo wabunge kupinga na kuhujumu waziwazi juhudi na jitahada za utekelezaji wa ahadi za mh Rais. Kama vile Kubana matumizi ya fedha za bunge kwa wabunge kutosafiri kwenda nje ya nchi kwa kisingizio cha kwenda kukagua ujenzi wa balozi zetu ilihali tunajua wao sio mainjinia wa majengo na pesa hizo kuelekezwa katika kutengeneza madawati ya wanafunzi na kila mbunge wa jimbo atapewa madawati 600 kwa ajili ya jimbo lake. Hivyo tunaamini wabunge nao walitoa ahadi zao kwa wananchi wao kwahiyo tunaomba na tunawashauri wajikite katika kutekeleza ahadi walizowaahadi wananchi wao kuliko kufanya malumbano,hujuma dhidi ya jitihada za utekelezaji wa ahadi za mh Rais.
Sote tunajua kauli mbiu ya mh Rais ni “Hapa Kazi Tu”  anataka awamu ya tano watu wafanye kazi, lakini bunge  lilipokulinaoneshwa moja kwa moja kwenye television tulikuwa tukishuhudia mijadala isiyo na tija kwa taifa, na zaidi Bunge lilikuwa uwanja wa kampeni za kisiasa,Vijembe, Kejeli, Mipasho na Vitimbi mpaka kufikia wao wenyewe kuliita bunge, “ Silly Season” na wengine wakiliita Bunge Comedy hivyo bunge kukosa Tija kwa Taifa na kupoteza kabisa maadili na kusudio la wananchi kufuatilia mijadala ya bunge letu hadi wengine hususan vijana kuacha kufanya kazi na kutumia muda mwingi kuangalia bunge kujifunza yasiyokuwa na tija kwa Taifa letu. Sisi kama Jukwaa tunawashauri wabunge wasijikite kwenye bunge kuoneshwa live bali wapige kazi kwa mustakali wa maendeleo ya Watanzania, na Wananchi watajua tu. Imefikia hatua Wabunge wanagoma kuchangia hoja bungeni kwa sababu tu familia , marafiki, ndugu na jamaa zao hawatawaona live. Sababu nyingine ni kuwa serikali haina Mwongozo na inatumia inatumia mwongozo wa awamu ya nne, sheria sio vacuum ndio maana Mawaziri hata kama bado hawajapewa mwongozo bado wanaendelea kutumia instruments za mwongozo iliyopita na kupata mwongozo mpya na bora ni mpaka serikali ifanye utafiti.
Pia Ukawa wameendelea kuhujumu shughuli za bunge kwa kuwazuia wabunge wao wasiende kwenye kamati mbili za bunge za PAC na LAAT na kusabisha kamati hizo kukosa uongozi.
Tunaishauri serikali nayo shughuli zake zote zitakazokuwa zinaenda moja kwa moja (live) zifanyike jioni au siku za mapumziko ya kitaifa.
Kwa kuhitimisha ndugu wana habari, tukirejea kauli ya Mh Mbowe na Ukawa wakijinadi kuwa mh Rais anatekeleza Ilani yao,sasa tunashangazwa na vitendo vyao vya ghafla vya kuanza kupinga na kujihujumu wao wenyewe kwa kutekelezwa kwa Ilani yao, tunapatwa na mashaka na nia yao katika Taifa hili na uenda wakawa wanatumika na Mafisadi na watu wasiokuwa na nia njema na taifa hili maana hata ile agenda ya ufisadi hatuisikii tena, Pia waache tabia ya kususa hata kama kasi ya Mh Rais ni kali ili tusiendelee kuwakosesha wananchi haki zao kama tulivyoona pale Zanzibar baada ya Chadema kuwashawishi Viongozi wa CUF kususia na  kuwazuia wana CUF  kushiriki uchaguzi  wa marudio na kuwapelekea kukosa uwakilishi ilihali wao wana wawakilishi ndani ya bunge.
Jukwaa tunaomba na tunatoa ushauri kwa Uongozi wa Bunge, kuchukua posho na ikiwezekana kukata mishahara ya wabunge wote wasioshiriki vikao na shughuli za bunge na fedha hizo zipelekwe kwenye matumizi mengine ya kutatua kero za wananchi ikiwemo upatikanaji wa chaki mashuleni.
Ndugu wana habari, Kuna baadhi ya watu pamoja na Wabunge wa Ukawa wakiongozwa na mh Mbowe, wamekuwa wakilalama kwamba Rais anakiuka katiba na sheria za kwa kubadili matumizi ya fedha. Sheria ya Usimamizi wa Bajeti {Appropriation Act ya 2015 (6) Waziri wa Fedha anapewa mamlaka ( Baada ya Maagizo au Mashauriano ya ndani ya serikali) Lakini pia Katiba inamruhusu Rais ndani ya miezi baada ya kuchaguliwa kuweza kubadili matumizi ya fedha . Bajeti ikishapitishwa inakuwa ya serikali na endapo itakuwa imezidi , fedha zile Waziri anaweza kuzipangia matumizi mengine au akasaini na Rais akatangaza maana ndiye anayewateua.
Jukwaa linaiomba serikali itusaidie maana wao wana mkono mrefu ili tujue dhamira zao ni nini? Ikiwa kama Mpango wa serikali ni Kutoa elimu bure, ikiwa Mpango ni kufufua Viwanda,Ikiwa Mpango ni Kubana Matumizi, Ikiwa Mpango ni Kupambambana na rushwa, ikiwa Mpango ni kujenga barabara, Ikiwa 41% ya Bajeti ni kwa ajili ya Maendeleo nk kama hawayataki haya kwa Watanzania, Je hawa wana Agenda gani nyuma?
Mwisho Mh Rais alitoa Rai, “Atakayejaribu kumkwamisha Atakwama Yeye

Imetolewa 24/04/2016 na :-
MTELA MWAMPAMBA 0755 17 89 27­, 0627 94 95 15
…………………………………
KATIBU JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA
 

TAMKO JUU YA MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE
TAMKO JUU YA MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE
TAMKO JUU YA MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE
 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger