Test Footer
WARAKA No. 2 WA MHE. SPIKA KUHUSU UGONJWA WA CORONA
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, March 17, 2020 | 1:33 AM
UVCCM CHAMWINO WAJAZA FOMU KWA NIABA YA BARAZA LA WADHAMINI
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, March 9, 2020 | 2:56 AM
MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, July 10, 2018 | 7:08 AM
*MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE KATIKA JIMBO LA DODOMA MJINI*
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde* leo amepokea mifuko ya Saruji 724 yenye thamani ya *Tsh 10,000,000* kutoka *Benki ya CRDB* kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa,Nyumba za Walimu na matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Dodoma Mjini.
Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji,Mkurugenzi CRDB Tawi la Dodoma *Bi Rehema Hamis* amesema kwamba Benki ya CRDB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano chini ya *Mh Rais Dr John Pombe Magufuli* na uchapakazi wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde katika kuboresha miundombinu ya Elimu.
Akipokea mifuko hiyo ya saruji,Mbunge Mavunde ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo ambao utalenga kupunguza changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa 1035 katika Jimbo la Dodoma Mjini ambapo kwa hivi sasa anaendesha kampeni maalum ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi na kwa kuanzia mfuko wa Jimbo umetoa matofali 32,000 na mifuko ya Saruji 2,560 kwa kata mbalimbali.
TANZIA: Mwanajeshi wa Tanzania auawa na wengine watano hali ni mbaya
Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, June 6, 2018 | 3:31 AM
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christine Mndeme , leo tarehe 3/6/2018 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru Na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Christopher Ole Sendeka.
Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, June 3, 2018 | 10:13 AM
*RUVUMA NA MWENGE WA UHURU*
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma *Mhe Christine Mndeme* , leo tarehe 3/6/2018 amekabidhiwa *Mwenge* wa Uhuru Na Mkuu wa Mkoa wa Njombe *Mhe Christopher Ole Sendeka* .
Mwenge wa *Uhuru,* ukiwa Mkoani *Ruvuma* unatarajia kuzindua Jumla ya *miradi 70* yenye thamani zaidi ya Shilingi *bilioni 11.* itafunguliwa,kutembelewa na kuwekwa mawe msingi.
Mwenge wa *Uhuru* utakimbizwa Halmashauri Nane za Mkoa wa Ruvuma.
*Mwenge wa Uhuru kwa Maendeleo CHANYA ya Mkoa wa Ruvuma !*
AJALI MBAYA YAUWA MAAFISA WA SERIKALI
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, May 22, 2018 | 12:43 AM
KIFO CHA AKWILINA NI MTAJI WA SIASA KWA WANASIASA UCHWALA WA TANZANIA.
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, February 20, 2018 | 2:22 AM
NB:- "Haya ni Maoni yangu yasihusishwe na mtu wala taasisi yoyote!"
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AKWILINA MAHALA PEMA PEPONI! AMINA…….!!
SIKU YA USAFI,UVCCM WAMEFANYA USAFI OFISI YA DC CHAMWINO.
Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, August 26, 2017 | 8:31 AM
LEO SIKU 26/08/2017 SIKU YA USAFI UVCCM CHAMWINO WAMEFANYA USAFI OFISI YA DC CHAMWINO.
Kwa Heshima Kubwa Vijana wa UVCCM leo wameshiri Kufanya Usafi Pamoja na DC Mama Jesca Nyamoga wa Chamwino akiwa na Wasaidizi wake DAS na Afisa Tarafa wa Chilonwa Ndg Mfaki na Maafisa Wengine.
Akizungumza na Vijana DC amewasisitizia Vijana Kuhakikisha Wanajitolea zaidi ktk Shughuli zakijamii ili Kujifunza na Kujenga Network yao kwani Ndio Mirango ya Fulsa kwao.
Nao Vijana wameahidi Ushirikiano kwa Chama na Serikali hii ya Awamu ya Tano, kwani wanayo imani Kubwa na Utendaji Kazi Wa Awamu Hii Kuanzia kwa Rais mpaka Kwa Watendaji wa Ngazi ya Chini Kabisa.
Nae Katibu wa Vijana Wilaya ya Chamwino Ndg Peter Dafi Akishukuru kwa Niaba ya Vijana UVCCM Chamwino, Amesema Kazi Kubwa ya Vijana Nikuhakikisha Wanayafanya yale Yote ambayo Vijana wanapaswa Kuyafanya kwa Umri wao wa Ujana kwani Vijana ni Taifa La Leo na Vijana Ni Jeuri ya Chama.
Ivo kwa hali na Mali, Kwa Shida na Raha Tutakitumikia Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake.
Dafi amemuahidi DC kumpatia Ushirikiano wa Kila Namna ili Kujenga Chamwino Bora na Taifa Moja lenye Amani na Upendo Ili Kuishi kwa amani na Furaha tele.
#ChamwinoYetu
#TanzaniaYetu
#UzalendoKwanza
#HapaKaziTu
WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO.
Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, May 4, 2017 | 8:40 AM
WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO.
Na.Catherine Sungura, WAMJW
Dodoma
Watanzania hususan wale wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano wanatakiwa kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha vyeti vipya
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati alipofika kupata huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa bungeni hapa
Waziri Mwijage amesema duniani ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza wananchi wake kwa kuugua ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya zetu,pamoja na kwamba nchi yetu haina mgonjwa wa homa ya manjano
Aidha amesema maambukizi ya ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake ni ghali sana na inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke reheni maisha yako
Hata hivyo aliwatahadharisha wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma nje ya nchi ni vyema wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa njia nyingine kwani kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi za kimataifa zina uwezo wa kusoma alama zetu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na vyeti vingi ambavyo vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata chanjo,hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanapata chanjo hizo kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye milipuko wa homa za manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa kubadilisha vyeti vya zamani hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti vya zamani havitatambulika tena.
UMMY MWALIMU -UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA UENDE SAMBAMBA NA USALAMA WA CHAKULA
Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, March 8, 2017 | 12:52 AM
UMMY MWALIMU -UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA UENDE SAMBAMBA NA USALAMA WA CHAKULA
Katika kuadhimisha Siku ya wanawake Duniani 2017, leo Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) ameungana na wanawake wa Mkoa wa Singida, katika Manispaa ya Singida. Akiwa katika shughuli za maadhimisho hayo mkoani Singida Waziri Ummy ametembelea mradi wa Wanawake wa IR VICOBQ Ititi Singida ambao ni wa kuzalisha viazi lishe.
Akiwa katika Mradi huo wa wanawake wa kuongeza thamani ya mazao, Mhe Ummy amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa kuwekeza katika shughuli za wanawake ambao ndio wazalishaji wakubwa wa Chakula na bidhaa za viwandani.
Mhe Ummy ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaongeza jitihada ktk kuwapatia fursa na mikopo ili waweze kushiriki kikamilifu ktk uzalishaji wa bidhaa za viwandani na bidhaa za chakula.
Huduma za CT Scan, MRI na Mammograph kupatikana Benjamin Mkapa Hospital, Dodoma
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, February 28, 2017 | 8:44 AM
Huduma za CT Scan, MRI na Mammograph kupatikana Benjamin Mkapa Hospital, Dodoma
Dodoma. 28-02-2017
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe Ummy Mwalimu amewathibitishia wananchi wa kanda ya Kati wakiwemo watumishi wa umma wanaohamia mkoani Dodoma kuwa huduma zote za matibabu ya kibingwa sasa zitapatikana katika Hospitali ya Kisasa ya Benjamin Mkapa iliyopo UDOM - Dodoma.
Mhe Ummy ameyasema hayo leo wakati alipokagua ufungaji wa Vifaa vya kisasa katika Hospitali hiyo ikiwemo CT Scan, MRI, Mammograph na Digital X-ray mashines ambazo zimefungwa katika Hospitali hiyo. Mhe Ummy ameagiza kazi ya ufungaji na majaribio ikamilike haraka ili huduma zote muhimu zitolewe kwa ukamilifu kuanzia tarehe 1 April 2017
Akiongea mbele ya Waziri Ummy, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dr Chandika alieleza kuwa kazi ya ufungaji vifaa hivyo imekamilika na kesho tar 1 Machi wataalam wa vifaa wataviwasha kwa majaribio. Pia tayari wameshawaandikia Wataalam wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (Tanzania Atomic Energy Commission) kuja kukagua vifaa hivyo ili kujiridhisha endapo ufungaji wa vifaa hivyo umekidhi vigezo vya Tume hiyo.
Hata hivyo, Mkurugenzi alieleza kuwa Changamoto kubwa iliyopo sasa ni Watumishi. Akijibu hoja hiyo, aliahidi kufanya uhamisho wa ndani wa Wataalam kutoka Wizarani ili kuimarisha huduma katika Hospitali hii sambamba na kuendelea kuwasiliana na Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kupata watumishi wakutosha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watumishi ya Hospitali hiyo.
Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyoko UDOM imefungwa vifaa vya uchunguzi vya Tiba vya kisasa ikiwemo MRI ambao ndio ya kisasa zaidi kupatikana eneo la ukanda wa Afrika Mashariki.
Kukamilika kwa Hospitali hii kutakuwa na mchango mkubwa sana kwa wananchi wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Manyara na Iringa ambao wanalazimika kwenda umbali mrefu kufuata huduma za matibabu ya kibingwa hasa Dar es salaam.
-----
HOME GROUND HOTEL SASA KUWA NA LIVE BAND KILA JUMAMOSI.
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, December 19, 2016 | 12:35 PM
HOME GROUND HOTEL SASA KUWA NA LIVE BAND KILA JUMAMOSI.
Hotel ya Kisasa nayakijanja ipatikanayo Sinza Mugabe, Kila Pamekuwa na Music Mzuri, Chakula na Vinywaji Bila Kusahau Vyumba Visafi na Vizuri kwa Kupumzika utokapo safarini ama kupumzika kama unahitaji utulivu.
HOM GROUND HOTEL Kwa sasa Kila Jumamosi Patakuwa na LIVE BAND .
Bila Kusahau Mechi Zote za Kimataifa Zitaonyeshwa ktk Luninga za Vyumbani na Zote zilizoko Bar na Restaurant.
Karibu sana Hom Ground Hotel Kila Siku kwa Chakula, Nyaa Choma, Vinywaji nk....!
UFAFANUZI WA KUTUMBULIWA DKT MWELE NA KUHUSISHWA KWA WAZIRI UMMY MWALIMU.
Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, December 17, 2016 | 11:39 PM
UFAFANUZI WA SAKATA LA KUTUMBULIWA KWA DKT MWELE MALECELA NA WAZIRI UMMY MWALIMU KUHUSISHWA NALO.
Ndugu Zangu Ni Masaa Kadhaa yamepita Tangu Mh Rais Alipoamua Kumtumbua Aliekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya NIMR. Watu wengi wamesema maneno mengi kwa hisia nyingi, nakwakutumia Sababu zao Nyingi pia kulingana na vyanzo vyao vingi vya Habari juu ya sakata hili.
Watanzania nivema tukatuliza Munkali kila linapotokea jambo. Na Vema zaidi tukaamua Kuishi Maisha ya uhalisia na kuacha kuishi maisha ya Matukio.
Utaratibu wa Shirika la Afya Dunia (WHO) wa Kutoa Taarifa za Magonjwa ya KULIPUKA utaratibu nikwamba! Tatizo linapotokea Nchini Taarifa Hupelekwa Wizara ya Afya, Wizara hujiridhisha na Taarifa hizo, Kisha Wizara hutoa Taarifa katika Shirika la Afya Duniani (WHO) Kisha nao WHO Mpaka Wajilidhishe Ndio Directer General wa WHO anatoa Taarifa kwa Dunia kuwa Nchini Tanzania au Nchi Fulani kuna Gonjwa Fulani la Mlipuko.
Sasa Dada Yangu Dkt Mwele Alifanya Utafiti Yeye Mwenyewe na Taasisi yake ya NIMR Nakutoa Taarifa yeye Mwenyewe Bila hata Kuishirikisha Wizara ya Afya ambapo ndio Boss Wake.
Manake NIMR Iko Chini ya Wizara ya Afya inapaswa kutoa Taarifa zake Wizarani kabla haijapeleka kwa vyombo vya habari hasa jambo Nyeti kama hilo.
Watanzania wenzangu Tufahamu Kuwa Kila Kazi ina Mipaka yake.
Damage ya Dadangu Dkt Mwele Malecela kutangaza uwepo wa Ugonjwa imekuwa kubwa Sana, Mpaka imepelekea CDC/ Wamarekani kutoa hiyo alert ya ZIKA Nchini. Hii ni baada ya Tamko la juzi la Taasisi NIMR.
Tunaweza Shabikia kusema maneno mengi nakuona kama Dkr Mwele hajatendewa Haki na Mh Rais Kumtoa katika Nafasi yake, lakini Hiyo nikwasababu wengi walalamikaji Hawajui Athali za Kusema ama Kutoa Taarifa zisizo na Ukweli kwa Taifa Letu.
Lakini Pia Taarifa Ya NIMR Haikufuata Utaratibu Wa Kiutendaji baina ya Wizara na Taasisi hiyo, Kama Utaratibu ungelifuatwa basi Tusingefikia huko, Kwani kabla yakuita Waandishi wa Habari Wizara ingejilidhisha na isingetoa Taarifa kabla haijatoa Taarifa WHO kwani ndio Utaratibu wa Kutoa Taarifa kwa Umma ama kwa Dunia kwa Magonjwa haya ya Milipuko.
Mh. Rais ameamua kumpumzisha Dkt. Mwele Malecela kwa kutumia Sifa na Sababu zake yeye kwa kutumia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama nk...
Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu aliwajibika kama waziri kwa nafasi yake kwa kutoa ufafanuzi na taarifa yakiwizara kutokana na uhalisia wa taarifa za Mfumuko wa Magonjwa Nchini.
Na ilikuwa niwajibu wake kama Waziri kufafanua Jambo lile baada yakuwa tayali limekuwa halina Ukweli. Ivo Si Vizuri Kumuhusisha Waziri wa Afya na Maamuzi ya Mh Rais kwani Rais ni Taasisi na Anafanya kazi kwa Umakini Mkubwa na sio kufanya kazi kwa Mihemko nakutaka kuwafurahisha Mawaziri wake.
Waziri wa afya Mh Ummy Mwalimu kusema kuwa ndie aliemponza Dkt Mwele ama kumchongea kwa Rais kama baadhi ya watu walivyoanza kusema huko mitandaoni mimi nasema Waziri Alitimiza wajibu wake kama Waziri wa Afya, Na Mh Rais Kaifanya kazi yake yakumuwajibisha Mtumishi wake kama Rais.
Tukumbuke zama hizi ni zama za Hapa Kazi tu! na sio Mchezo mchezo na Porojo.
Niwatakie Wakati Mwema.
Ni Mimi
Peter L. Dafi
Mtetezi wa Wanyonge.
0713302823
Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu Amefanya Semina kwa Waandishi wa Habari kufanya Mazoezi.
Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, December 15, 2016 | 8:22 AM
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa semina kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari,shinikizo LA juu la damu na moyo.
Katika kuelekea uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima Afya itakayozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu tarehe 17/12/2016 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam kuanzia Saa 12.30 asubuhi
Uzinduzi huo utatanguliwa na matrmbezi ya hiari ya kilomita 6.
#AFYAYAKOMTAJIWAKOFANYAMAZOEZILANDAAFYAYAKO
MWIGULU NCHEMBA AWAONYA MADREVA WANAOACHA MAGOGO,MAWE NA MATAWI YA MITI KWENYE BARABARA.
Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, November 23, 2016 | 1:10 AM
MWIGULU NCHEMBA AWAONYA MADREVA WANAOACHA MAGOGO,MAWE NA MATAWI YA MITI KWENYE BARABARA.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba akemea madereva wanaoacha mawe na magogo barabarani baada ya kutengeneza magari yao
Aagiza wakamatwe kila wanapobainika kufanya kosa hilo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amekemea vikali jambo hilo kwakati wa kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Singida kilichokaa jana tar 22.11.2016.
Akiongea wa masikitiko,Mwigulu amesema tabia hii imeshamiri kwa baadhi ya madereva kuweka mawe makubwa, magogo au matawi ya miti punde magari yanapokuwa yameharibika. Kibaya ni kwamba wanapotengeneza magari yao huyaacha mawe au magogo katikati ya barabara na kuondoka zao. Hali hii imekuwa ikisababisha ajali na imekuwa chanzo kikuu cha uharibifu wa barabara.
Nukuu, "tuwe wastaarabu na wazalendo katika matumizi ya barabara, kuna madereva wanaweka Mawe na Magogo makubwa barabarani wanapoharibikiwa na magari, wakishatengeneza wanaondoka bila kuondoa mawe hayo au magogo hayo, huu sio uungwana, tabia hii inaharibu barabara zetu zilizojengwa kwa gharama kubwa na ni chanzo cha ajali"
Fikiria eneo la mlimani au kwenye kona kali, watu wanaweka Mawe makubwa yanawasaidia kutengeneza, wakimaliza hawayaondoi barabarani na kuondoka wanaacha palepale, huu sio ustaarabu, ni sawa na mtu aliyejisaidia naakacha choo bila kuflash, un civilization ya hali ya juu"
naagiza kwa nchi nzima Askari chukuen kumbukumbu kila magari yanapoharibika, wakiondoka bila kuondoa mawe wasilianeni popote watakapokuwa wamefika wakamatwe na wafike kwenye mkono wa sheria kwa kutengeneza mazingira ya ajali na kuharibu barabara" lazima tuwe na uzalendo na ustaarabu kwenze utunzaji wa barabara zetu na kujali usalama wa Raia wetu.
Ziara ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Jijini Arusha
Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, November 16, 2016 | 6:53 AM
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA. (CCM)
Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu Taifa lilimefanya Ziara Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Ziara hiyo ililenga mambo mbalimbali pamoja na :
1.Uzinduzi wa Tawi jipya SAUT ARUSHA. Pamoja na kupokea kwa Wanachama wapya wa Tawi hilo 165.
Sambamba na IMANI KUBWA YA WASOMI KWA RAIS hatimaye kuamua kujiunga na Chama chake Cha Mapinduzi(CCM).
2.Hali ya kisiasa sambamba na Utoaji wa Mikopo. Shirikisho limebaini bado changamoto zipo hasa mikoani hususani za Mikopo. Hivyo kuwaomba watumishi wa bodi ya Mikopo kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo hayo pamoja na kuwataka wakuu wa Vyuo kuhimiza Majina ya wanafunzi/Wanufaika wa Mikopo kuwasilishwa Haraka Bodi kama alivyosema Mhe Prof Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekinologia.
3.Uhai wa Shirikisho matawini na Mikoani. Shirikisho Taifa kilamewataka Wanachama kutimiza wajibu wao kama ilivyoainishwa ndani ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha shirikisho linakuwa kimbilio la wanafunzi hasa katika Matawi katika kutatua changamoto zilizopo Mavyuoni. Hilo litaongeza Ari kwenye Matawi yetu na kuongeza Wanachama.
Shirikisho Taifa limewakumbusha Wanachama wake Wasomi kuendelea na kuongeza Nguvu katika kukisemea Chama Chao CCM, pamoja na Kazi Kubwa anayoifanya mhe Dkt John Pombe Magufuli kutekeleza AHADI na ILANI ya CCM. Hasa Ongezeko la Mikopo ya Vyuo Vikuu sambamba na Kubaini Mikopo hewa, Elimu bora,Elimu Bure, Kubaini Wanafunzi Hewa hivyo kuokoa Fedha nyingi, Matumizi yasiyo ya lazima na Ongezeko la Mapato KODI,Uwajibikaji,Maadili ya Utumishi wa Umma,Ndege Mpya za kisasa na Kumpongeza RAIS na Serikali kwa Ujumla.
4.Uchaguzi uliopo Shirikisho na kuhamasisha makada kushiriki. Shirikisho Taifa limetatua changamoto zilizopo Kilimanjaro hasa juu ya mkanganyiko uliokuwepo juu ya kuitangaza nafasi ya mwenyekiti Mkoa wa Kilimanjaro kuwa WAZI na Makada wajitokeze kuwania nafasi zilizopo wazi.
5.Ziara hiyo ilijikita kuelekeza kufanyika kwa Uhakiki Wanachama waliopo na kupokea Taarifa za Kiutendaji pamoja Changamoto zilizopo Mikoani pamoja na Kutoa Rai juu ya Wanachama Hewa na kuelekeza Uhakiki ufanyike kuanzia ngazi ya Matawi.
6.Shirikisho Taifa kuzindua LIBRARY MAALUM " Online library" library itakuwa BURE na itajumuisha vitabu vyote pamoja na Kiswahili. Library itaisaidia Usomaji wa Vitabu kupitia Mtandao na itarahisisha upatikanaji wa vitabu na kuongeza Maarifa zaidi kwa Wasomi na hata Wakufunzi/Walimu. Shirikisho itazindua library hiyo hivi karibuni. Sambamba na Database yake.
Shirikisho Taifa limehamasisha na kuwataka Wanachama walio maliza masomo kujiunga kwenye vikundi ili kujiunga na Programu ya Uzalendo "UZALENDO NI VITENDO" Ilikujitolea kufanya shughuli za kimaendeleo na kutoa mchango katika Taifa. Mfano Ujenzi wa Madarasa, Matundu ya Vyoo ya Shule pamoja na Mabweni na Nyumba za Walimu.
Pamoja na kuwapongeza Viongozi wa Shirikisho wa Mikoa ya Arusha kwa kazi nzuri na Kilimanjaro kwa kujitoa na kufanya vizuri katika kufanikisha Ziara hiyo.
Imeandaliwa na kutolewa.
Mtumishi Wenu
Daniel zenda.
Kny;K/Katibu Mtendaji
Shirikisho-Taifa.
HOTUBA YA UMMY MWALIMU KWA WABUNGE KTK SEMINA YA UDHIBITI WA KIFUA KIKUU.
Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, November 10, 2016 | 11:50 AM
HOTUBA YA MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, KATIKA SEMINA YA WABUNGE KUHUSU UDHIBITI WA UGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE, 8 NOVEMBA, 2016.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Mhe. Job Ndugai,
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania -
Mhe. Tulia Akson,
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania -
Mhe. Andrew Chenge,
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania -
Dkt. Thomas Kashilila,
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe,
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Mhe. Peter Serukamba,
Wenyeviti wa Kamati mbali mbali za Bunge,
Waheshimiwa wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi kukushukuru kwa dhati kwa kutupatia fursa nyingine ya kuongea na Waheshimiwa wabunge wa Bunge lako Tukufu kuhusu masuala ya maendeleo katika sekta ya Afya na kwa siku ya leo ajenda yetu ni ‘Janga la ugonjwa wa kifua kikuu’ nchini mwetu.
Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwa kukubali kuhudhuria semina hii muhimu ili kupata fursa ya kuliangalia tatizo la Kifua kikuu kwa kina na kuishauri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto juu ya maboresho muhimu ili kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya Kifua kikuu. Nawaahidi kwamba, Wizara yangu itazingatia ushauri wa Waheshimiwa wabunge katika kuboresha mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi, kwa hotuba nzuri uliyoitoa hivi punde wakati wa ufunguzi wa semina hii. Ni kweli kabisa, kifua kikuu au TB ni ugonjwa hatari, yatupasa kufanya juhudi za kipekee na za ziada ili kuiokoa jamii yetu na janga hili. Aidha, naomba nimpongeze Mhe. Peter Serukamba, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii kwa salamu zake na maneno yenye hekima kubwa juu ya wajibu wetu katika kukabiliana na tatizo hili la kifua kikuu hapa nchini mwetu.
Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii pia, kuwashukuru wale wote waliohusika katika kuandaa semina hii ikiwa ni pamoja na wadau wetu wa maendeleo wa shirika la kimataifa la kupambana na Kifua kikuu la KNCV linalosimamia mradi wa Challenge TB unaofahiliwa na USAID.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyobainisha katika hotuba yangu ya bajeti kwa mwaka 2016/17, katika mwaka huu wa fedha wa 2016/17 Wizara inaweka juhudi za kipekee katika kuongeza wigo wa mapambano dhidi ya kifua kikuu na kuboresha mikakati ya uibuaji wa wagonjwa wapya ili kupunguza ukubwa wa tatizo la Kifua kikuu hapa nchini mwetu. Aidha katika tamko langu wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu Duniani mnamo mwezi Machi, 2016 nilitoa wito wa kumtaka kila mtanzania na taasisi mbali mbali kujiunga pamoja na kuisaidia serikali kutimiza azima yake ya kutokomeza kifua kikuu hapa nchini katika miaka 20 ijayo.
Mheshimiwa Spika, Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa: “Tuungane Kutokomeza Kifua Kikuu” kwa lugha ya kiingereza: “Unite To End TB” Kauli mbiu hii inaweka msukumo wa kipekee kwa nchi yetu kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya kifua kikuu ili kuibua wagonjwa wengi zaidi, kuwaweka katika matibabu na kuzuia maambukizi mapya. Kauli mbiu hii inatoa pia chagizo kwa nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ikiwemo Tanzania, katika utekelezaji wa mkakati mpya (Global End TB Strategy 2016-2035) wa Dunia wa utokomezaji wa kifua kikuu ifikapo mwaka 2035.
Mheshimiwa Spika, Mkakati huu unatutaka kuongeza kasi ya juu kabisa katika kuutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu, ili kuwafikia wahitaji na wagonjwa wote, kupunguza kasi ya idadi ya wagonjwa wapya kwa asilimia 90, kuwatibu na kuwaponyesha wote, kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kifua kikuu kwa asilimia 95 na kukomesha masumbukizo yote yatokanayo na kifua kikuu katika jamii yetu.
Mheshimiwa Spika, Kifua kikuu kinaleta madhara ya kiafya na huongeza umasikini katika jamii. Nchini kwetu takriban watu 160,000 huugua kila mwaka na ni wagonjwa 62,180(39%) tu wanagunduliwa na kuwekwa katika matibabu. Miongoni mwa hawa tunaowaweka kwenye matibabu asilimia 90 hupona kabisa. Kwa misingi hiyo, Wizara yangu imeona litakuwa jambo la kheri kukutana na Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge lako Tukufu, kama wadau wakuu na wawakilishi wa wananchi ili kulijadili janga hili angalau kwa muda huu mfupi tulioupata.
Tunahitaji ushiriki wa kila mtu katika vita hii na kama kauli mbiu inavyoonyesha “TUNAHITAJI KUUNGANISHA NGUVU”. Bunge letu ni chombo nyeti na ushiriki wake unaweza kufanya tofauti kubwa na kuleta tija katika maboresho ya mkakati wa azma ya Taifa letu kuelekea Tanzania isiyo na TB.
Mheshimiwa Spika, Takwimu zinatuonyesha ya kuwa, takribani asilimia kati ya 30 na 50 ya watanzania wote tayari wameambukizwa Kifua kikuu, yaani watu wapatao million 25. Kwa maneno mengine ni kwamba, pengine hata nusu yetu hapa ukumbini tayari tunayo maambukizi ya TB na endapo kinga yetu itashuka kwa sababu yoyote ile, ugonjwa wa TB utatukumba na kuhitaji kupatiwa matibabu sahihi na kwa wakati.
Mheshimiwa Spika, Kama tulivyoona, kifua kikuu ndiyo ugonjwa pekee ambao watanzania wengi zaidi wanaishi na vimelea vyake mwilini. Hii ina maanisha na kueleza wazi hatari tuliyo nayo katika jamii yetu. Yatubidi kuchukua hatua za makusudi kuongeza uwekezaji wa rasilimali nyingi zaidi katika mapambano hayo ili kukiokoa kizazi hiki na kijacho. Makundi ya wazee, watoto, watu wanaoishi na maambukizo ya VVU, watu wenye magonjwa hatari ya kudumu kama vile kisukari na kansa, watu walio migodini, wanafunzi katika shule za bweni, wafungwa magerezani, kambi za wakimbizi hawa wote wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua ugonjwa wa kifua kikuu.
Mheshimiwa Spika, Ni matarajio yetu ya kuwa mkutano huu, utatoa fursa kwa Waheshimiwa Wabunge kupata uelewa zaidi juu ya hali ilivyo, ukubwa wa tatizo la kifua kikuu hapa nchini na kuwawezesha kuona ni namna gani wanaweza kushiriki katika mapambano dhidi ya janga hili la kifua kikuu. Kuna masuala ya kuhimiza ushiriki kikamilifu wa wananchi, Halmashauri zetu na Taasisi mbali mbali katika vita ya udhibiti wa kifua kikuu. Yapo pia masuala ya bajeti ya kifua kikuu; kwa miaka mingi imekuwa ikitegemea wafadhili kwa zaidi ya asilimia 90 na sasa tunaona wakipunguza misaada yao. Yote haya yanahitaji msukumo wa kisiasa na kisera pia.
Mheshimiwa Spika, Katika semina hii tutapokea mada mbili kuu, moja itawasilishwa na Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na nyingine ataitoa Mhe. Dkt Faustin Ndungulile, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Mwenyekiti wa kamati ya UKIMWI, mjumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na mwanachama mwanzilishi wa Bunge lako Tukufu katika “Global TB Caucus pamoja na Afican TB Caucus”. Mada hizi zitachokoza tu na Waheshimiwa watapata muda wa kutosha kuchangia kwa kutoa ushauri na kuuliza maswali pale ambapo kunahitaji ufafanuzi. Mada hii itafuatiwa na uzinduzi rasmi wa “Tanzania TB Caucus”.
Mheshimiwa Spika, Naomba nimalizie kwa kushukuru sana tena sana kwa kutupatia fursa hii adimu ya kujadili janga la TB na Waheshiwa Wabunge na napendekeza kikao hiki kiweze kuweka maazimio ya Waheshimiwa Wabunge kuhusu ushiriki wao na Bunge lako Tukufu katika mapambano dhidi ya TB na kuyapa sura ya utekelezaji katika ngazi zote.
Baada ya kusema hayo narudisha nafasi kwa Mwenyekiti wa Bunge ili kuendelea na taratibu nyingine.
Asanteni kwa kunisikiliza.
KWAHERI CHUMA CHA PUA JOHN SAMWELI SITTA
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, November 7, 2016 | 12:05 AM
KWAHERI CHUMA CHA PUA JOHN SAMWELI SITTA.
Sikuwai Kuwa Rafiki yako wala Msaidizi wako.
Niliwai kuwa Mpenzi wa Misimamo yako na Mwanafunzi wako usiemjua Mpaka pale siku nilipokutamkia kuwa Baba! Najifunza mengi toka kwako na Ukasema "KARIBU DAFI KWA KUJIFUNZA ZAIDI MAADILI NA UWONGOZI, KWANI NYIE HASWAA NDIO VIONGOZI WA KESHO"
Awali nilipata Taabu sana Kukufahamu kwa Hadhi na Nyadhifa ulokuwa nazo iliniwia ugumu sana kupata wasaa wakukutana nakuzungumza na wewe CHUMA CHA PUA.
Namshukuru Rafiki yangu na Kaka yangu RC @paulmakonda kwa Mara ya Kwanza alinishika Mkono nakunileta Nyumbani kwako Masaki akanitambulisha kwako na nikachota Hekima na Busara zako.
Hakika Sintosahau Kila Tamshi lililotoka katika Kinywa chako, kwani kila neno lilikuwa ni Somo na Darasa Lenye Zaidi ya PHD ambazo husomwa Darasani.
Nilizaliwa Nzega Mkoani Tabora, Nilipokuwa nakuwa nakupenda Sides niliambiwa! Sikonge kuna Kiongozi mwenye Maono makubwa na vitendo vyakizalendo, Nilikuwa nikiwa nikipata Sifa na nakuona Utendaji wako mkubwa ndani ya Serikali na @ccmtanzania .
Hakika Wana Tabora Tumeondokewa na tumepungukiwa na Kiongozi Mahiri na Nguli wa Siasa kwa Mkoa wa Tabora ambae amejitahidi sana kuiweka Tabora katika Historia yakutoa Viongozi Bora kwa Taifa letu.
Nasema Poleni wana Sikonge, Pole wana Tabora, Pole Tanzania Pole Africa na Dunia Nzima, kwani John Samweli Sitta ni Mmoja tu Wakitofauti. na Hakuna Mwenye kuweza kuziba Pengo lake kamwe.
Nitaikumbuka Daima Falsafa yako ya KAZI KWA VIWANGO, wakakuita MZEE WA VIWANGO, Tanzania imeweka Historia yako ktk Vitabu Mpaka Dunia itakwisha, Daraja la Sarenda, Morogoro Road nk... Hizi ni kazi zako mpaka leo ni bora zaidi na zaidi.
Kwa Ubora wako ulipewa Majina yakishujaa mengi sana, CHUMA CHA PUA, MZEE WA VIWANGI nk....
KWA PAMOJA NAUNGANA Mh. RAIS John Pombe Magufuli KUTOA POLE KWA FAMILIA YA MZEE SITTA KWA KUONDOKEWA NA MPENDWA WAO, POLE KWA SPIKA WA BUNGE, POLE KWA MH MBUNGE WA SIKONGE MAMA SITTA, POLE KWA KAKA NA RAFIKI YANGU MH MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI MH BEN SITTA, POLENI SANA FAMILIA YA MZEE SITTA KWA MSIBA HUU MZITO.
BWAMA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
APUMZIKE KWA AMANI....!
DAS MWAKIPOSA AFUNGUA MASHINDANO YA MPIRA WA PETE WA WASICHANA.
Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, November 6, 2016 | 9:02 AM
DAS MWAKIPOSA AFUNGUA MASHINDANO YA MPIRA WA PETE WA WASICHANA.
Na Peter Dafi (Arusha)
Katibu Tawala wa Arusha mjini Bw David Mwakiposa, amezindua Mchezo wa Mpira wa Pete wa wasichana.
Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Babtist Jijini Arusha. Mashindano hayo ya Mpira wa Pete "Netball" yanayohusisha timu nane za Arusha.
DAS Mwakiposa akizungumza na Mabinti na Wanawake zaidi ya Mia mbili (200), waliohudhulia mchezo huo. Amewasihi watumie timu hizo kuunda vikundi vya ujasiriamali, ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri ya JIJI la Arusha ya asilimia10% kwa Wasichana na Wavulana.
Katika zoezi hilo alitoa Jezi na Mipira, lakini pia aliahidi kuzifanyia kazi changamoto zao walizowasilisha mapema katika Risala yao.
Aidha, jana alikuwa mgeni Rasmi katika mashindano ya Riadha yanayohusisha Mbio za CROSS COUNTRY. Mashindano yanayoshirikisha wakimbiaji wakike na wakiume, ambapo aligawa zawadi ya fedha na viatu kwa washindi wa kwanza hadi wa sita.
Mwakiposa amewasisitiza vijana hao kuwa wazalendo na kupenda michezo, kwani michezo ni ajira na zaidi hutangaza Nchi. Aliwapongeza Vijana ambao wameiwakilisha vyema Nchi hii katika olimpiki mwaka huu hususani kijana aliyekuwa wa tano.
Aliwaeleza kuwa muda wote wakimuhitaji kwa ushirikiano kamwe Ofisi yake haitasita kuwasikiliza ili kutatua Changamoto zao.
www.peterdafi.blogspot.com
WIZARA YA AFYA KUIMARISHA AFYA YA UZAZI,MAMA,WATOTO NA VIJANA
Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, November 3, 2016 | 6:34 AM
WAZARA YA AFYA KUIMARISHA AFYA YA UZAZI,MAMA,WATOTO NA VIJANA
Ni heshima kubwa kwa nchi yetu kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 3 wa Wafadhili wa Kimataifa wa Afya ya Mama na Mtoto (Global Financing Facility (GFF) for Every Woman, Every Child).
Wizara ya Afya tunajivunia kutengeneza na kukamilisha Mpango wa Pili wa Taifa wa Kuimarisha Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana (The National Roadmap Strategic Plan to Improve Reproductive, Maternal, Newborn and Adolescent Health in Tanzania - ONE PLAN II), ambao ndio Nyenzo ya Kutafuta Uwekezaji wa Rasilimali Fedha katika kutekeleza shughuli mbalimbali kwenye eneo hili. GFF ni mojawapo ya wafadhili waliowekeza katika Mpango huu.
Hivyo jana usiku wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wajumbe wa GFF na Wawekezaji katika Afya Duniani nilitangaza rasmi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, World Bank/GFF tutaboresha Vituo vya Afya 100 *VituovyaAfya100Kuboreshw* ili kuviwezesha kutoa huduma muhimu za uzazi na za dharura ktk Halmashauri mbalimbali nchini.
Ktk kila kituo cha Afya tutajenga Theatre, Maabara ya kuhifadhi damu, Wodi ya Wazazi na Nyumba 1 ya Mtumishi.
Vigezo vitakavyotumika kuchagua Vituo hivyo ni pamoja na;-
1. Vikwazo vya kijografia katika eneo husika mfano uwepo wa mto, mlima au barabara zisizopitika kipindi cha mvua,
ii. Idadi ya wa wananchi ktk eneo husika.
iii. Muda wa kusafiri (masaa) hadi Kituo cha Afya au Hospitali yenye Huduma za uzazi za dharura
iv. Idadi ya Zahanati zitakazotoa Rufaa kwa ajili ya huduma za dharura
v. Idadi ya Wajawazito wanaozalishwa.
Nimedhamiria tuanze utekelezaji wa Mpango huu haraka iwezekanavyo. Kwani kukamilika kwa mpango huu itakuwa ni mchango mkubwa sana wa Serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli ktk kuboresha Huduma za Afya hasa afya ya mama, uzazi na mtoto. Hadi sasa, ktk Vituo vya Afya 489 vya umma ni takribani vituo 113 tu ndio vinatoa huduma muhimu za uzazi na za dharura zinazokidhi viwango. (Basic Emergence Obstetric & Newborn Care (BEMONC) and Comprehensive Emergence Obstetric & Newborn Care -CEMONC).
Nikiwa na dhamana ya kuongoza Wizara ya Afya lakini pia Mwanamke na Mama huu utakuwa ni mchango wetu mkubwa katika kuboresha huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto hasa kwa wanawake wenzangu waliopo katika maeneo magumu kufikika.
Kwa niaba ya Serikali, Wizara ya Afya na Wanawake wa Tanzania tunawashukuru sana World Bank/GFF pamoja na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation, Canada, DFID, JICA, Norway na USAID kwa kufanikisha hili.
Kwa Pamoja Tunaweza Kupunguza Vifo vya Wanawake Wajawazito nchini. *Tushirikiane*!
Ummy Mwalimu, MP.
WAMJW
Dar es salaam
3. Nov 2016










