Home » » JACQULIN WOLPER KUKIJUA KIARABU.

JACQULIN WOLPER KUKIJUA KIARABU.

Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, June 8, 2012 | 7:12 AM

 Jacqueline Wolper ameamua kumuajiri mwalimu (ustadhi) wa kumfundisha mwenendo mzima wa kuijua dini yake ya Kiislam ambayo amejiunga nayo hivi karibuni.

  Wolper alisema kuwa amelazimika kutafuta mwalimu ili aweze kuujua mwenendo na maadili ya dini hiyo kabla hajaanza kujumuika na waumini wenzake katika ibada za kila siku.

Wolper sasa anaishi Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, ustadhi huyo atakuwa akienda nyumbani kwake kumfundisha na anaamini hatachukua muda mrefu kuijua dini hiyo.

“Nimeamua kutafuta ustadhi wa kunifundisha, ila sijaanza kujumuika na Waislam wenzangu msikitini kwa kuwa bado sijashika mafundisho vizuri.

“Kwa kweli sioni tofauti kati ya Ukristo na Uislam kwani wote tunamuabudu Mungu labda tofauti zaidi ni mavazi marefu ambayo sasa najitahidi kuyavaa ili kuendana zaidi na taratibu ya dini yangu mpya tofauti na nilivyokuwa mwanzoni,” alisema Wolper
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger