Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 taasisi inayoendesha mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon itawazawadia wadau waliofanikisha mbio za mwaka 2012 ambazo zilipambwa na mlimbwende na mcheza sinema maarufu kutoka Marekani Deidre Lorenz.
Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon mwaka huu zilishughudia wakimbiaji kutoka nchi mbalimbali zakiongezeka na kuzifanya kuendelea kuwa mbio zinazopendwa na wakimbiaji wasio na ujuzi wa kukimbia (Fun Run)!
Mbio za mwaka huu zitakumbukwa kwa mambo matatu makubwa.
Mosi ni ujio wa mblimbwende na mcheza sinema maarufu Deidre Lorenz kutoka katika jiji la mapesa la New York City au linavyojulikana kama “The Big Apple”
Lorenz anayemiliki kampuni yake mweneywe ya kutengeneza filamu ya Thira Films LLC alidhihirisha kwa vitendo uchangiaji wake wa kuutangaza mlima Kilimanjario kuwa ni mali ya asili ya taifa letu.
Ujio wa Lorez aliyekwisha kucheza filamu nyingi zikiwamo Santorini Blue, The Big Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi kulileta hamasa kubwa kwenye mbio za marathon.
Jambo la pili ni zawadi ya kukimbia kilometa 50 ambayo Chris Wilde aliyoipatia Tanzania kwa ajili ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Wilde mganga msaidizi kutoka katika jiji la Minnesota alikimbia mbio hizo kwa kila kilometa iliwakilisha mwaka mmoja wa uhuru.
Mkimbiaji huyo kijana aliahidi kuja tena Tanzania kukimbia kilomta 51 mwakani kusheherekea miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika pamoja na miaka 23 ya kuanzishwa kwa Mt. Kilimanjaro marathon mwaka 1991.
Jambo la tatu kubwa ni mbio za Mt. Kilimanjaro kutimiza miaka 22 tangu zilipoanzishwa na Marie Frances mwaka 1991. Frances mkazi wa jiji la matajiri la Bethesda lililoko nje kidogo ya jiji la Washington DC nchini Marekani.
Kuzawadiwa kwa wadau waliochangia kufanikisha mbio hizi ni mkakati wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 kujipambanua kama taasisi inayojali na kusheshimu uchangiaji wa kuiendeleza tasnia ya riadha. Hii ni mara ya kwanza kwa tasisi ya michezo kutoa zawadi kwa wadau walioichangia katika kufanikisha melengo yake!
Taarifa hizi na:.... l
Grace Soka
AfisaUhusiano
Mt. Kilimanjaro Marathon 1991
Post a Comment