Home » » NDEGE YA ATC YAPASUKA KIOO BALAA TUPU

NDEGE YA ATC YAPASUKA KIOO BALAA TUPU

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, July 19, 2012 | 2:51 AM

Habari za uhakika zinadai kuwa ndege ya ATCL namba TC 100 ambayo ilikuwa imeondoka Dar mapema asubuhi ya leo (July 18) kuelekea Mwanza ikipitia KIA imepasuka kioo.
Taarifa zimedai kuwa kioo hicho kilipasuka wakati ndege hiyo ikijiandaa kwenda Mwanza baada ya kuwa imeshatua KIA. Kioo kilichopasuka ni kile cha pembeni kwa rubani upande wa kushoto kwa mujibu wa vyanzo.
Kutokana na tukio hilo ndege hiyo ilizuiwa kuruka hadi pale marekebisho ya kioo hicho yangefanyika. Haijajulikana iwapo imesharuhusiwa ama bado. Source: Jamii Forums.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger