Home » » TANGA WAZIKOMALIA NGUMI MPAKA KIELEWEKE.......!!!!

TANGA WAZIKOMALIA NGUMI MPAKA KIELEWEKE.......!!!!

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, August 16, 2012 | 8:44 AM



Tanga  wazikomalia ngumi





Kampuni  ya  Mwanzoa Promotions ya Tanga chini ya mkurugenzi wake Ally
Ommar inaendeleza mkakati wake wa kunyanyua vipaji vya wanamichezo wa
jiji la Tanga hasa katika mchezo wa ngumi kwa mapambano ya ubingwa wa
Afrika mashariki yatakayopigwa siku ya iddi mosi na iddi pili. Ally
omar’Mwazoa’ akikimuhakikishia katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini
Ibrahim kamwe”bigright” kuwa maandalizi ya mapambano yote yamekamilika
na mabondia  wapo katika hali nzuri ya ushindani ambapo siku hiyo ya
iddi mosi katika ukumbi wa CCM HALL, Said mundi wa Tanga atazipiga na
Habibu pengo wa Dar es salaam katika kugombania ubingwa wa Taifa wa
TPBC uzito wa super feather raundi kumi,nae jumanne Mohamed wa Tanga
atazipiga na ali bugingo wa Dar es salaam uzito wa light weight raundi
kumi,katika uzito wa super fly Haji juma(Tanga) na Mwaite juma(Dsm)
watacheza raundi nane na mapambano mengineyo mengi ya utangulizi wa
mabondia wa watakaotoka katika vitongoji mbalimbali vya jiji la tanga.
Na siku ya idi pili katika ukumbi wa pweza kutakuwa na pambano kubwa
la ubingwa wa Afrika mashariki na kati, kati ya Alen Kamote wa Tanga
na bondia toka Uganda ni pambano la raundi kumi pia zuberi kitandula
wa Tanga atazipiga na Sadiki Abdul azizi wa Dar es salaam raundi
kumi,jay jay ngotiko wa tanga atapigana na bondia juma afande toka
morogoro pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi ya mabondia
wakongwe wa tanga na wale chipukizi takribani mabondia wote wa kulipwa
wa jiji la Tanga watashindana hakuna atakaekosa kazi labda awe na
matatizo binafsi. mwazoa alimalizia kwa kusema hizi ni mbio za
kuyakusanya mataji yote ya Tanzania na Afrika mashariki yaje mkoani
Tanga na tayari mpaka sasa ina mabingwa sita wa Tanzania na mmoja wa
Afrika mashariki.

imetolewa na;
ibrahim Abbas kamwe
ibrakamwe@yahoo.com
+255 713 501991
+225 767 501991

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger