Home » , » Jaribio la 3 la Nuklia, Korea Kaskazini

Jaribio la 3 la Nuklia, Korea Kaskazini

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, January 24, 2013 | 5:23 AM



Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kombora la masafa marefu Disemba 2012
Korea kaskazini imethibitisha kuwa inamipango ya kufanya jaribo lengine la kinuklia litakalojumuisha kurusha roketi za masafa marefu.
Hatua ya Korea inajiri siku mbili baada ya Baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa, kulaani jaribio lengine la Nuklia lililofanywa na nchi hiyo. Inaarifiwa pia hatua hiyo imechukulia na Korea Kaskazini tokana na vikwazo ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa.
Tume ya kitaifa ya ulinzi imesema kuwa jaribio hilo linafanywa kwa kuzingatuia adui mkubwa wa nchi hiyo , Marekani.
Iliongeza kuwa ndio njia pekee ya nguvu kuweza kukabiliana na Marekani.
Baraza la usalama la umoja wa mataiafa, limesema kuwa halina mipango ya kuficha tarifa kuwa Pyongyang's imekuwa ikitekeleza majaribio hayo na Marekani ni mojawapo ya mataifa yanaoenekana kama adui wa korea kaskazini .
Korea kaskazini imedai kuwa njia ya kipekee ya kakabilaina na washington ni kupitia silaha.
Balozi wa marekani katika Umoja wa Matifa, wa korea kaskazini Glyn Davise amesema kuwa Marekani haitosita kuchukua hatua iwapo majaribio hayo yatafanywa.
Davies, alisema kuwa jaribio hilo la nuklia ni kosa kubwa wakati Korea Kusini ikijaribu kuishawishi Pyongyang kutofanya vitendo vyovyote vitakavyozua hisia kali.
Baraza la Uslama pia liliongeza vikwazo dhidi ya nchi hiyo kufuatia jaribio lengine mwezi Disemba , jambo lililotazamiwa na nchi jirani za Korea Kaskazini kama jaribio lililoharamishwa la makombora ya masafa marefu.
Hata hivyo ilijitetea kwa kusema kuwa ililenga kuweka satellite katika anga ya juu kwa sababu za kiusalama.
Marekani na Korea Kusini zinahofia kuwa huenda nchi hiyo ikafanya jaribio lengine la tatu.
Mapema siku ya Alhamisi, waziri wa ulinzi wa Korea Kusini, alisema kuwa nchi hiyo inejiandaa kwa jaibio la Nuklia ikiwa kiongozi wake atauidhinisha.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger