Zaidi ya watalii 19
wakiwemo waingereza na wafaransa ,wamefariki Kusini mwa Misri baada ya
puto la joto walimokuwa kulipuka katika mji wa Luxor.
Ripoti zinaarifu kuwa kulikuwa na watalii ishirini katika puto hilo.Duru zinasema kuwa takriban maiti wanane walipatikana katika eneo la tukio.
Mji wa Luxor uko kwenye ukingo wa mto Nile, makao ya kale ya pharao. Ni eneo lenye sifa tele kwa watalii
Mwakilishi wa makamapuni manane ambayo yanatengeza putu hizo, katika eneo la Luxor alisema kuwa mlipuko wa gesi ulitokea wakati puto hilo likiwa umbali wa futi alfu moja kutoka ardhini.
''Kulikuwa na abiria 20 kwenye puto wakati wa ajali hiyo. Mlipuko ulisikika na abiria 19 wakafariki. Abiria mmoja na rubani wa puto hilo walinusurika,'' alisema mwakilishi huyo, Ahmed Aboud.
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza iliambia BBC kuwa inatafuta taarifa kutoka kwa wenzao nchini Misri kuthibitisha taarifa za majeruhi waingereza.
Chanzo BBC Swahili
Post a Comment