Afisaa wa polisi anayeongoza uchunguzi dhidi ya mwanariadha Oscar Pistorius anakabiliwa na makosa saba ya jaribio la mauaji.
Polisi wamethibitisha hilo dhidi ya afisaa
Hilton Botha,ambaye amaekumba na wakati mgumu kujibu maswali katika kesi
ya dhamana ya mkimbiaji huyo inayoendelea nchini Afrika Kusini.Bwana Pistorius, mkimbiaji mlemavu na bingwa wa mihcezo ya Paralympic, amekana kosa la mauaji ya mchumba wake, Reeva Steenkamp, aliyekuwa na umri wa miaka 29.
Kesi yake inatarajiwa kuendelea hii leo ambapo mahakama inastahili kuamua ikiwa itamwachilia mwanaridaha huyo kwa dhamana.
Msemaji wa polisi, Neville Malila, alisema kuwa afisaa huyo, Det Botha na maafisa wengine wawili, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mwezi Mei.
Bwana Malila alisema kuwa ilidaiwa alipokuwa anaendesha gari la serikali , watatu hao waliifyatulia risasi basi iliyokuwa imewabeba abiria.
Duru zilisema kuwa ushahidi alioutoa Det Botha siku ya Jumatano ulionekana kupatia nguvu upande a mashtaka na kisha kutoa matumaini ya Pistorius kupata dhamana .
Aliambia mahakama kuwa milio ya risasi aliyosikia ilikuwa ishara ya Pistorius kuwa na miguu yake bandia .
Hii bila shaka ilitofautiana na taarifa yake ya awali iliyotolewa na Pistorius kuwa alikuwa anatembea akiwa amavelia miguu yake bandia na kuchukua bunduki kwa sababu alihisi kuwa mtu alikuwa amevamia nyumba yake.
Watatu hao walikamatwa mwaka 2011
Bwana Malila aliambia shirika la habari la Reuters kuwa mashtaka dhidi ya afisaa huyo, yalikuwa yametupiliwa mbali lakini mahakama ikayarejesha Jumatano na mwendesha mashtaka baada ya polisi kusimama kizimbani.
Haijulikani ikiwa afisaa huyo ataendelea kuhusika na kesi inamkabili Oscar Pistorius.
Post a Comment