Wachimba migodi 14 nchini Afrika Kusini, wamejeruhiwa wakati wa makabiliano makali kati ya vyama viwili hasimu vya wafanyakazi hao mjini Rustenburg
Mwezi Agosti mwaka jana, eneo la Rustenburg lilikuwa kitovu cha migomo ya wachimba migodi ambapo polisi waliwaua 34 miongoni mwa wale waliokuwa wanaandamana.
Ghasia katika mgodi wa Marikana ndiizo zilikuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu enzi ya ubaguzi wa rangi.
Hata hivyo hakuna polisi wowote walihusika na makabiliano hayo. Haya yalithibitishwa na msemaji wa polisi Thulani Ngubane.
Makabiliano yanadhaniwa kutokea kati ya chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa migodini na shirikisho la wachimba migodi na wajenzi.
Walinzi katika migodi hiyo waliingilia makabiliano hayo kujaribi kuyatuliza na wakati wakifanya hivyo ndipo wakawajeruhi wafanyakazi 13 na walinzi wanne.
Baadhi ya watu walikatwa kwa mapanga na silaha zingine kali.
Watatu kati ya waliojeruhiwa wanaaminika kuwa katika hali mbaya.
Mwaka jana migomo ya wafanyakazi wa migodini ilienea hadi katika migodi mingine kote Afrika Kusini.
Post a Comment