Home » » Wafanyakazi wa kutoa misaada wafungwa jela

Wafanyakazi wa kutoa misaada wafungwa jela

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, February 13, 2013 | 12:12 AM



Eric Breteau na mwenzake walikataa kwenda mahakamani kujieleza mwaka 2007
Wafanyakazi wawili wa misaada nchini Ufaransa, wamefungwa jela miaka miwili kila mmoja kwa kujaribu kuwahamisha watoto 103 nchini Ufaransa kutoka Chad mwaka 2007.
Eric Breteau, aliyeanzisha shirika la misaada la Zoe's Ark, pamoja na mshirika wake, Emilie Lelouch, walihukumiwa bila wao kuwa mahakamani ingawa walifika mjini Paris kwa hukumu.
Wafanyakazi wengine wanne wa shirika hilo walipokea vifungo vya nje vya kati ya miezi sita na mwaka mmoja.
Shirika la Zoe's Ark lilitozwa faini ya pauni 86,000 na hata kufungwa.
Watoto waliokuwa wanahamishwa waliaminika kuwa mayatima kutoka nchini Sudan hususan jimbo la
Darfur ambalo linakumbwa na vita.
Lakini baadaye iligunduliwa kuwa wanatoka Chad na wengi wao wana familia zao.
Katika kisa kilichowashangaza wengi nchini Ufaransa, washtakiwa walikamatwa nchini Chad wakijaribu kuwaweka watoto hao kwenye ndege iliyokuwa inaelekea Ufaransa mwaka 2007.
Walihukumiwa jela miaka minane pamoja na kufanyishwa kazi ngumu nchini Chad lakini wakapelekwa Ufaransa, baada ya mawasiliano na Rais wa Chad mwezi Machi mwaka 2008.
Washukiwa sita walipatikana na hatia ya kwenda kinyume na sheria kwa kufanya kazi kama shirika wakala la kuasilisha watoto, kuingiza watu nchini Ufaransa kinyume na sheria pamoja na ulaghai waliofanyia familia 358 waliotarajia kuasili watoto.
Wawili hao bwana Breteau na Bi Lelouch, waliokuwa wanaishi nchini Afrika Kusini, walikataa kwenda mahakamani mwanazoni mwa kesi yao, mapema Disemba, wakisema kuwa hawako tayari kujieleza.
Lakini waliwasili mahakamani Jumanne kusikiliza uamuzi wa mahakama walipopewa kifungo cha miaka miwili gerezani , faini ya Euro 50,000 kila mmoja na kupigwa marufuku kufanya kazi yoyote inayowahusu watoto wadogo. Wakili wao alisema kuwa watakata rufaa.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger