Home » » Watu 35 wafariki katika ajali ya basi Kenya

Watu 35 wafariki katika ajali ya basi Kenya

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, February 27, 2013 | 5:47 AM



Basi hilo lilikuwa linaelekea Mandera na Garissa
Takriban watu 35 wameuawa katika ajali ya barabarani karibu na mji wa Mwingi Mashariki mwa Kenya.
Duru za polisi zilisema kuwa wengi wa waliofariki walikuwa wanafanya kazi mjini Nairobi, na walikuwa wanarejea makwao kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya Jumatatu.
Farah Aden Ali, aliyenusurika kifo alisema kuwa basi hilo lilikuwa limejaa watu kupindukia na lilianguka baada ya dereva kupoteza mwelekeo.
Barabara nyingi nchini Kenya ziko katika hali mbaya na vile vile hali ya mabasi mengi ni mbaya.
Afisaa wa trafiki Samuel Kimaru alisema kuwa takriban abiria 35 walifariki na wengine 50 kujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Bwana Aden Ali aliambia BBC kuwa vikundi vya uokozi viliwasili katika eneo la ajali masaa manne baada ya ajali kutokea hali iliyosababisha waliokuwa wamekwama ndani ya basi hilo kufariki.
Basi lilikuwa limejaa watu na lilikuwa linaelekea katika miji ya Mandera na Garisa
Ali alisema kuwa dereva alikuwa na matatatizo na gia ya basi hilo tangu kundoka Nairobi
Alisema alikuwa amelala lakini aliamka muda mfupi baada ya ajali kutokea.
''Dereva alipoteza mwelekeo. Alikua anajaribu kulirejesha basi barabarani , lakini likaanguka kwa upande,'' alisema Ali.
Babaraba za Kenya huwa na msongamano mkubwa wa magari hususan kabla ya uchaguzi mkuu huku wafanyakazi wa miji wakielekea mashinani kupiga kura.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger