Home » , » Balozi Afrika Kusini alalamikiwa: amekuwa akiwadhalilisha kwa kuwapiga vibao...

Balozi Afrika Kusini alalamikiwa: amekuwa akiwadhalilisha kwa kuwapiga vibao...

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, March 7, 2013 | 12:06 AM

 Balozi wa Tanzania nchini humo, Radhia Msuya


WATANZANIA wanaoishi nchini Afrika Kusini, wamemlalamikia Balozi wa Tanzania nchini humo, Radhia Msuya kwa kuwanyanyasa na kuwadhalilisha. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Watanzania hao wamesema Balozi huyo amewatengea siku mbili tu za wiki za kuonana naye, ambapo siku zilizobaki zimetengwa kwa ajili ya watu wa mataifa mengine.

Mbali na kuwapunja muda wa kuwasiliana naye, pia Balozi huyo amekuwa akiwadhalilisha kwa kuwapiga vibao na aina nyingine ya udhalilishaji.

Akizungumzia tukio hilo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Michael Haule alisema Wizara haina taarifa za malalamiko hayo.

"Niseme tu wewe ndio unanipa hizi taarifa wala hatukuwa nazo na naomba nipe muda ili nilifanyie kazi halafu nitakujulisha, kwa kweli tungekuwa na taarifa tungekuwa tumeshaitolea maamuzi maana hii ni serious issue (taarifa muhimu).

"Yaani kweli Balozi anadhalilisha watu kwa kuwapiga hadi wanaume, hii haiwezekani, ahsante kwa taarifa na nakuahidi kulifanyia kazi kwa mapana yake," alisema.


BALOZI AKIWA RAIS ZUMA
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger