Rais Xi Jinping, rais wa Uchina, ametia saini mikataba kadha na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania mjini Dar-es-salaam.
Hapo awali alipokelewa kwa ngoma na mizinga.
Rais Xi alitia saini mikataba 17 ya uchumi na utamaduni, mojawapo ni kuhusu ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo pamoja na reli itayoungana na reli nyengine za Tanzania.
Akizungumza ikulu mjini Dar-es-salaam, kiongozi wa Uchina alisema ziara yake ni ishara ya uhusiano mwema kati ya nchi mbili hizo ambao umeendelea tangu ulipoanza wakati wa Rais Julius Nyerere na Mao Zedong.
Safari yake barani Afrika inaonesha umuhimu wa Afrika kwa Uchina, kuwa ni chanzo cha madini na nishati na piya soko kwa bidhaa za Uchina.
Rais wa Uchina anatarajiwa kutoa hotuba muhimu Jumatatu kuhusu uhusiano baina ya Uchina na Afrika.
Inatazamiwa kuwa atapooza maoni kwamba Uchina inaingia Afrika ili kunufaika na madini tu ya bara hilo.
Uchina ni ya pili katika uwekezaji nchini Tanzania, baada ya Uingereza.
Bwana Xi piya anapanga kuzuru Afrika Kusini ambako viongozi wa mataifa ya uchumi unaochipukia, BRICS, watakutana Jumaane mjini Durban.
Baada ya hapo anapanga kuzuru Congo.
Post a Comment