kijana
Godfrey Masharo mkazi wa mjini Iringa akivuja damu baada ya
kuchomwa kisu kifuani na watu wasiofahamika usiku wa leo wakati
akitoka kujirusha disco
Hivi ndivyo alivyochomwa kisu kijana huyo.
Hapa akivuja damu akiwa nje ya kituo cha polisi kabla ya kupelekwa hospitali ya mkoa wa matibabu zaidi
WATU
wasiofahamika wamemvamia na kumchoma na kitu chenye ncha kali
kifuani mkazi wa mjini Iringa Godfrey Masharo (pichani) .
Tukio
hilo limetokea jana usiku majira ya saa 11 alfajiri wakati kijana
huyo akitoka kujirusha katika kumbi za starehe mjini hapa.
Akizungumza
kwa tabu na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kijana
huyo anadai kuwa watu hao watatu ambao hawafahamiki kwa majina
walimvamia na kumchoma na kitu hicho chenye ncha kali kifuani na
kukimbia .
Alisema
kuwa tukio hilo limetokea eneo la Miyomboni barabara kuu ya Iringa
-Dodoma jirani na jengo la Hazina Ndogo ya mkoa wa Iringa .
Hata
hivyo alisema kuwa msaada wake ulitoka kwa wasamaria wema ambao
walimkuta eneo hilo akiwa ameanguka kwa kupoteza fahamu na kukimbizwa
katika kituo cha polisi kabla ya kupelekwa Hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi .
NA FRANCIS GODWIN BLOG
Post a Comment