Home » » MWANAMUZIKI KUTOKA MAREKANI MAYA ATUA TANZANIA HOUSE OF TALENT (THT)

MWANAMUZIKI KUTOKA MAREKANI MAYA ATUA TANZANIA HOUSE OF TALENT (THT)

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, March 6, 2013 | 6:41 AM

 Meneja wa Biashara wa Nyumba ya vipaji Tanzania,THT,  Kemilembe Mutahaba, akizungumza na mwanamziki kutoka Marekani,
Meneja wa Biashara wa Nyumba ya vipaji Tanzania,THT,  Kemilembe Mutahaba, akizungumza na mwanamziki kutoka Marekani, Maya Azurenca ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku saba katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya mwanamke duniani. Maya alitembelea THT leo ambapo alishiriki mjadala kuhusu changamoto zinazowakabili wasanii wanawake katika soko la muziki Tanzania





THT yaandaa mjadala kuhusu changamoto zinazowakumba wasanii wa kike, pamoja na mwanamziki wa kimarekani,Maya Azurenca.
Katika kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya kimataifa ya wanawake duniani, leo Nyumba ya vipaji Tanzania, THT, imeandaa majadiliano kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wasanii wa kike hapa nchini, mjadala uliohusisha wasanii wa kike kutoka THT,wasichana kutoka nyumba ya kulelea watoto yatima wa KIWOHEDE na mwanamuziki kutoka Marekani, Maya Azurenca ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku saba.
Mjadala huo pia ulitoa fursa kwa kinadada walio kwenye muziki, kama Mwasiti, Trio, Linah, Vumi na Rachel kuelezea changamoto na uzoefu wao katika tasnia ya muziki.
Mjadala huo uliwapa nafasi kina dada wanamuziki wa Tanzania kujifunza kutoka kwa Maya, ambaye ni mwanamuziki wa muda mrefu kutoka Marekani.
 
Maya Azurenca akibadilishana mawazo na wasanii kutoka THT
Maya ambaye pia ni balozi wa utamaduni, ameimba nyimbo mbalimbali zinazohusu haki za binadamu na pia amefanya matamasha nchi nyingi duniani kwa lengo la kuhamasisha kuhusu haki za binadamu.
Katika mjadala huo, wasichana waliozungumza walisema kinadada katika tasnia ya muziki wanakumbwa na changamoto nyingi na pia ni vigumu kwa waimbaji wa kike kupata fursa ya kufanikiwa kulinganisha na wenzao wakiume.
Wakizungumza katika mjadala huo, mwanamuziki wa kundi la kike la TRIO, Angela Karashani, alielezea changamoto kubwa ambayo anakumbana nayo ni watu kudhani wao ni wahuni hasa kwa kuwa wanajihusisha na muziki.

The Trio, alipowatembelea ofisini kwao leo asubuhi.
‘Ukiwa mwanamuziki wa kike kwanza huwa ni shida sana kupata sapoti, lakini pia watu wengi wanachanganya muziki na uhuni, ukiwa mwanamuziki wengi wanakufata wakidhani wewe ni mhuni pia’ alisema Angela.
Mwanadada Maya aliwapa chanagamoto kinadada hao wanamuziki kwa kuwaambia kuwa waweke juhudi katika muziki na hakika watafika mbali.
‘Kitu kikubwa ambacho nimejifunza kwenye maisha yangu ya muziki na ningependa kuwaambia hapa ni kuwa kuwa mwanamuziki wa kike sio jambo rahisi, lakini kikubwa ni kuamini kile unachofanya na kuweka juhudi katika hilo na kujiamini’ alisema Maya.
Mwanamuziki huyo pia ametoa fursa ya kufanya nyimbo kadhaa na wanamuziki wa kitanzania wakati wa ziara yake hii hapa nchini ili kuwapa fursa ya muziki wao kusikika kimataifa zaidi.
Wakati huo huo pia, uongozi wa nyumba ya vipaji Tanzania, umetoa shukrani za pekee kwa ubalozi wa Marekani Tanzania ambao ndio wamewezesha safari ya mwanamuziki huyo hapa nchini.
 
Akiwa THT pia alipata fursa ya kushiriki mjadala kuhusu changamoto zinazowakabili wanamuziki wa kike hapa nchini.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger