Mabondia wawili wanaotarajia kupigana leo Ijumaa ratehe 8 Machi
kugombea ubingwa wa Afrika katika uzito wa Lightweight, Richard Commey na Bilal
Muhammed wamekutana leo katika zoezi la
kupima uzito na nusura wazipige kavukavu kama wasingeachanishwa na wasimamiszi
wa mpambano huo.
Richad ndiye aliyekuwa wa kwanza
kuwasili katika eneo la kupima uzito ambalo ni hoteli maarufu ya Coco Grove
Regency iliyoko karibu na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kutoka jijini Accra.
Alifuatana na meneja/promota wake Michael Amoo- Bediako na kocha wake Carl
Lokko.
Bilal naye aliingia muda mfupi
baadaye akifuatana na meneja pamoja na kocha wake Yebohey na kundi kubwa la
mashabiki wa kambi yake kutoka Bukom, Jamestown.
Mabondia wote Richard na Bilal
walifikia uzito wa kilo 59.9 na kutangazwa kufikia uzito unaokubaliwa na IBF
katika uzito wa mwepesi. Zoezi hili lilisimamiwa na Mtanzania Onesmo Ngowi
ambaye ndiye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya
Kati akisaidiwa na referii Rodger Barnor wa Ghana.
Mpambano huu utafanyika kesho
tarehe 8 Machi katika ukumbi wa Will Power Gym – City Engineers, Jamestown
jijini Accra ambapo Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika atajulikana
rasmi.
Post a Comment