Home » » Ujio wa Rais wa China, Xi Jinping nchini Tanzania - Machi 2013

Ujio wa Rais wa China, Xi Jinping nchini Tanzania - Machi 2013

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, March 26, 2013 | 2:46 AM


Rais Xi Jinping anafanya ziara ya kwanza barani Afrika tangu achaguliwe kuwa Rais. Kituo cha kwanza cha ziara yake ni Tanzania, pia atakwenda Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa BRICS halafu atakwenda Congo Brazzaville. Akiwa Tanzania atatoa hotuba kuhusu sera ya serikali yake kuhusu Afrika, na kuhusu Tanzania.

Kumekuwa na maswali mengi na ya msingi yanayoulizwa kuhusu ziara hii, hasa katika wakati huu ambapo ushirikiano kati ya China na Tanzania unaongezeka kwa kasi. Kwanza ni kwanini Tanzania imechaguliwa kuwa ya kwanza? Ni bahati tu, au kuna sababu maalum? Na pili watanzania wanatarajia au wanategemea nini kuhusiana na ziara hii?

Habari zinasema kuna miradi mikubwa ya ushirikiano itakayosainiwa, inagusa maswala ya uchumi, ujenzi, elimu na utamaduni.


Kwa sasa kuna mambo mengi yanayohusu ushirikiano kati ya nchi zetu mbili (Tanzania na China), hii ni fursa nzuri ya kuangalia uhusiano huu kwa pande zote.

Rais Xi Jinping anatarajiwa kufika jijini Dar es Salaam tarehe 24 Machi 2013 mchana, na anatarajiwa kutoa hotuba saa nne na nusu asubuhi katika Ukumbi mpya wa Mwalimu Nyerere, atakaoufungua siku hiyo.

Note: Maoni yenu yatasomwa LIVE redioni (Kupitia China Radio International) na hivyo kufanya uhariri binafsi (self editing) kutawasaidia wahariri wa JF kutopata kazi ngumu na hata watangazaji wa CRI kupata urahisi kuyasoma maoni yenu.

Sikiliza LIVE maoni yenu yakisomwa kwa kutembelea CRI LIVE


Beijing, Mar 18 (PTI)

China's new President Xi Jinping will visit Russia, Tanzania, South Africa and the Republic of Congo from March 22-30 in the first foreign tour after taking over as the head of state last week.

In South Africa, Xi would attend the Brazil, Russia, India, China and South Africa (BRICS) summit to be held in Durban.

Xi, who is also the General Secretary of the Chinese Communist Party, would also meet Indian Prime Minister Manmohan Singh on the sidelines of the March 26-27 summit.

Xi is making the visit at the invitation of Russian President Vladimir Putin, Tanzanian President Jakaya Mrisho Kikwete, South African President Jacob Zuma and President of the Republic of Congo Denis Sassou Nguesso, Chinese Foreign Ministry spokesperson Qin Gang said today.


Source: CCTV, Xi Jinping to visit Russia, African nations
Na Jamii Forum 
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger