Home »
kitaifa
» WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI AWASIMAMISHA MAAFISA 6 WA POLISI...
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI AWASIMAMISHA MAAFISA 6 WA POLISI...
Waziri wa mambo ya ndani Emmanue Nchimbi amewasimamisha kazi maafisa sita wa polisi kwa tuhuma mbalimbali.
waliosimamishwa ni Elias Mwita mrakibu Mwandamizi wa polisi aliekuwa
mkuu wa Upelezi mkoa wa Mbeya, Jacob Kiango Mrakibu wa polisi aliekuwa
msaidizi wa mkuu wa Upelezi mkoa wa Mbeya na Charles Kinyongo, mrakibu
msaidizi wa polisi aliekuwa mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa
Mbeya.
Hawa wamesimamishwa
kutokana na kufanya udanganyifu katika madawa ya kulevya yaliyoshikwa
jijini Mbeya mwaka jana ambao wanatajwa kuyaficha kupeleka kidhibiti cha
pakti za chumvi.
Askari wengine walipatikana na makosa ya
Kupiga na kuwabambikizia kesi zisizo na Dhamana wananchi kutokana na
Rushwa ni Peter Matagi, mrakibu Mwandamizi wa Polisi aliekuwa mkuu wa
upelelezi mkoa wa kagera.
Askari mwingine Renatus E Chalamila
kamishna mwandamizi wa polisi aliekuwa anasimamia Ajira za jeshi la
Polisi ambaye alidai na kujipatia fedha ili kutoa ajira kwa wanaotaka
kujionga na jeshi la Polisi.
Post a Comment