Gari # 6 ilipata pacha maeneo ya Iringa wakaiomba gari # 2 kuwasubiria ili waongozane ikiwa hizo zingine nne zikitangulia na safari ya Dar. Hivyo hizo ndipo zikawa nyuma na ilipofika maeneoCHALINZE ndipo lilitokea Gari kubwa la mafuta na Costa # 2 ya wanafunzi ndipo zilipogongana kwa uzembe wa Dereva mmoja kati yao kuovateki gari lingine ndipo zikagongana na Kosta # 6 kujigonga kwa nyuma ya gari # 2 kwani zilikuwa karibu karibu sana.
Dereva wa Kosta aliumizwa sana na mmbuluzo huo kuendelea kwa mstari na kujeruhi wanafunzi watatu ambapo mmoja wao aliekuwa nyuma ya kiti cha dereva ndie aliumia sana na kupoteza maisha baada ya muda mchache alipokuwa akikimbizwa Hosoitali ya Tumbi ambapo walipatiwa matibabu majeruhi wote wa ajali hiyo na Miili ya marehem kuifadhiwa katika mochwali ya Tumbi mpaka kesho yake.
Ajali hii ya kusikitisha iliuwa Dereva wa Kosta, Dereva wa Roli na Mwanafunzi wa DSJ ndugu Diedon Elianson ambae alikuwa ni mwanafunzi wa Diploma na waziri wa serikali ya wanafunzi DASJOSO,
Kiukweli kwa maelezo ya wanafunzi walimu na wadau wengine na ndugu pia wakimuelezea Marehemu ni kwamba, Jamaa alikuwa mchapakazi sana na mtu wakujituma sana hivo ni pengo kubwa sana kwa DSJ na DASJOSO pia.
Akizungumza na Peter dafi Baba mdogo wa marehemu alisema kuwa kijana huyu asiepungua miaka 24 alikuwa akimkabidhi familia yake nakusafri hata kuwalea wadogo zake na familia nzima hivo alisema haya kwa uchungu sana kuwa wamepoteza mbegu iliyo bora katika Familia yao.
Baba na Mama wanaishi Tabora, hivo imewalazimu kuja Dar mpaka nachapa taarifa hii Baba na Mama wamepanda ndege mkoani Tabora na ndege hiyo imepitia Nairobi kisha Dar hivyo wamechelewa kufika Dar.
Wanafunzi na waandishi wengine tunaombwa kujumuika na Familia ya Marehemu hapao kesho katika kumsindikiza mwenzetu katika makao ya milele, Misa itasomwa kanisa la PENTECOSTE mwananyamala karibu na CCM mwinjuma, huko Mwananyamala Kisiwani.
Kisha baada ya misa tutaelekea Makaburi ya Kinondoni, kwa ajili yakumpumzisha mwenzetu.
Hii ni Ratiba kamili ya Kesho
RATIBA YA KESHO NA MAZISHI
MUDA
|
TUKIO
|
MHUSIKA
|
01:00-05:00
|
Maandalizi ya asubuhi
|
Wakina Mama
|
05:00-05:30
|
Kula chakula
|
Wote
|
05:30-07:00
|
Safari kuelekea kanisani
|
Wote
|
07:00-08:30
|
Ibada na kuaga mwili wa marehemu
|
Wote/ Mchungaji
|
08:30-09:15
|
Kufika makaburini
|
Wote
|
09:15-09:30
|
Ibada fupi kaburini
|
Mchungaji
|
09:30-10:15
|
Mazishi
|
Wote
|
10:15-10:30
|
Kuweka mashada
|
Wahusika
|
10:30-10:35
|
Historia ya Marehemu
|
Mhusika
|
10:35-10:40
|
Hotuba ya wanafunzi
|
Mwakilishi
|
10:40-10:45
|
Hotuba ya Mkuu wa chuo
|
Mkuu wa chuo
|
11:45-10:50
|
Shukrani za familia
|
Mhusika
|
10:50-11:00
|
Kumaliza na Maombi
|
Kanisa
|
`11:00
|
Kuondoka Makaburini
|
Wote
|
`
Gari Kosta iliyosababisha kifo cha Mwanafunzi na Dereva
Dereva wa Kosta anaonekana hapo chini
Gari # 6 iliyokuwa ikiwafuata kwa nyuma hii ilijigonga kwa nyuma
No comments:
Post a Comment