Home » , » Wabunge 4 wa upinzani wakamatwa Arusha

Wabunge 4 wa upinzani wakamatwa Arusha

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, June 19, 2013 | 2:20 AM



Moja ya eneo ambalo lilikumbwa na shambulizi la bomu mjini Arusha Hili ni Kanisa Katoliki
Vurugu zimeendelea mjini Arusha ambapo jana polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kudhibiti mikutano ya hadhara kufuatia polisi kutangaza kutokuwepo kwa mikusanyiko ili kuimarisha usalama kufuatia mlipuko wa pili uliotokea mjini Arusha, baada ya mtu asiyejulikana kurusha bomu katika mkutano wa kisiasa
Wabunge wanne wa CHADEMA jana wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko bila kibali ambapo viongozi hao wa chama cha upinzani cha CHADEMA walikusanyika katika eneo lililotyokea mlipuko wa bomu la viwanja vya Soweto kwa malengo ya kutaka kufanya mkutano
Wabunge wanaoshikiliwa na polisi ni Tundu Lissu,Said Arfi , Joyce Mukuya mustafa Akoonay ambapo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kukamatwa kwa wabunge hao.
Hata hivyo kuna madai kuwa baadhi ya viongozi wengine wa chama cha Chadema wanasakwa na POLISI, wabunge hao wanatuhumiwa kuwahamasisha wafuasi wao kuwashambulia polisi kwa mawe wakati walipotakiwa kuondoka katika viwanja hivyo kwa hiari.
aidha polisi pia imekitaka chama cha CHADEMA kuwasilisha kile ilichodai kuwa ni ushahidi wa mtu aliyehusika na urushaji wa bomu hilo
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, inadaiwa kuwa bomu lililorushwa katika mkusanyiko huo lilitengenezwa nchini China. Kiongozi wa harakati dhidi ya tukio hilo Paul Chagonja amesema polisi wako tayari kupokea ushahidi kutoka kwa viongozi hao wa kisiasa wanaodai wana taarifa za mtu huyo aliye husika
Jana pia kumetokea vurugu kwa kile kilichodaiwa ni baada ya polisi kuzuia mkutano mwingine wa hadhara uliokuwa ukilenga kutaka kufanya ibada ya mazishi.

UPDATES
 Wabunge wa chadema ndio wanapelekwa mahakamani muda huu.

Ni Tundu lissu, mustafa Akonay, na mbunge na makamu mwenyekiti bara mzee Said Arfi pamoja na Joyce Mukya,

• Mashtaka ni mkusanyiko usio kuwa halali

• Zaidi ya watu 70 pia wamepelekwa mahakamani kwa makosa ya kukusanyika bila kibali.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger