Home » » Pembe za Ndovu zakamatwa Kenya toka Uganda

Pembe za Ndovu zakamatwa Kenya toka Uganda

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, July 4, 2013 | 5:55 AM



Bara la Asia lina soko kubwa sana la pembe za Ndovu
Pembe haramu za ndovu zilizokuwa zinasafirishwa kutoka Uganda hadi Malaysia, zimenaswa katika bandari ya Mombasa pwani ya Kenya.
Pembe hizo zilikuwa zimefunikwa kiasi cha kufanana na samaki waliokaushwa.
Mzigo huo wa takriban pembe 770 kutoka nchi Uganda, ulikuwa unapelekwa Malaysia.
Walanguzi hao pia walikuwa wamebeba samaki waliokuwa na harufu mbaya ambayo huwachukiza Mbwa maalum wa uchunguzi, kulingana na msemaji wa shirika la ulinzi wa wanyapori nchini Kenya Paul Udoto.
Pembe za Ndovu zina soko kubwa sana barani Asia, ambazo hutumiwa kwa vitu vya urembo.
Serikali ya Kenya iliharamisha biashara za pembe za ndovu mwaka 1989, huku viwango vya uwindaji haramu wa Ndovu vikipungua pakubwa, lakini pameanza kuonekana ongezeko la uwindaji haramu tena wa Ndovu katika miaka ya hivi karibuni.
Bwana Udoto alisema stakabadhi kuhusu pembe hizo zilolionyesha kuwa zilisafirishwa kutoka Uganda kwa gari tarehe 12 mwezi Juni.
Gari hilo kisha likaegeshwa katika kituo cha mafuta mjini Mombasa, eneo la kufanyia biashara hadi mzigo huo ulipofikishwa bandarini.
Thamani ya pembe hizo badi haijabainika kwa mujibu wa bwana Udoto.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger