Home » » Mh, John Tendwa Azungumzia Kustaafu kwake.

Mh, John Tendwa Azungumzia Kustaafu kwake.

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, August 7, 2013 | 2:53 AM


 
Na Mkinga Mkinga  (email the author)

Posted  Jumanne,Agosti6  2013  saa 22:30 PM
Kwa ufupi
  • Akizungumzia kuhusu viongozi wa vyama vya upinzani kupokea kwa nderemo kustaafu kwake, Tendwa alisema wala hashangai kuyasikia hayo kwani inaonyesha kwamba kazi yake alikuwa akiifanya vyema na mujibu wa sheria.

Harare. Siku moja baada ya kutangazwa rasmi kwamba aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amestaafu kwa mujibu wa sheria, amejitokeza na kueleza yaliyo moyoni mwake.
Katika mahojiano maalumu na Mwananchi jijini Harare jana, Tendwa alisema amepokea kwa mikono miwili kustaafu kutoka katika nafasi hiyo nyeti katika siasa za Tanzania, huku akisema anajiona mwenye bahati kufanya kazi na marais wawili katika nafasi yake.
Tendwa amefanya kazi chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na baadaye Rais Jakaya Kikwete. Nafasi ya Tendwa, imechukuliwa na Jaji Francis Mutungi ambaye alikuwa jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Akizungumzia kuhusu viongozi wa vyama vya upinzani kupokea kwa nderemo kustaafu kwake, Tendwa alisema wala hashangai kuyasikia hayo kwani inaonyesha kwamba kazi yake alikuwa akiifanya vyema na mujibu wa sheria.
“Unajua unapokuwa msajili na ukaona wadau wote wanakushangilia hapo ujue kuna tatizo kubwa, nimekuwa ninafanya kazi yangu vizuri sana kwa kuzingatia misingi ya sheria ambayo imewekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni,”alisema Tendwa.
Alisema kwamba, “Unajua kuvilea vyama ni kazi kubwa sana ndugu yangu, maana kuna wakati hata Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa wanasema ninaegemea na kuvipendelea sana vyama vya upinzani. Leo nimestaafu nasikia vyama vya upinzani vinasema kwamba nilikuwa nawapendelea CCM, hiyo inaonyesha kwamba nilikuwa ninafanya kazi yangu sawa sawa.”
Kitu gani ambacho Tendwa hatakisahau?
Alisema kwamba katika miaka yake 13 ambayo amekuwa msajili hatomsahau waziri mmoja wa CCM.
Hata hivyo, Mwananchi lilimbana kumtaja waziri huyo, lakini agoma kwa madai kwamba hapendi kuendeleza malumbano naye baada ya kustafu kwake utumishi wa umma.
Tendwa alisema katika utumishi wake, waziri huyo alikuwa akimpatia wakati mgumu sana kwa kumpakazia kwamba yeye ni mpinzani.
“Katika miaka yangu 13 ofisini sitaweza kumsahau huyo waziri maana alikuwa ananipakazia kwamba mimi ni mfuasi wa vyama vya upinzani. Ninamshukuru Mungu kwamba baadaye alikuja kuniomba msamaha, lakini ilikuwa imenisumbua sana katika kazi zangu,” alisema huku akionyesha masikitiko

Chanzo Mwananchi.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger